SAUDIA ARABIA WAISHANGAZA ARGENTINA

 Muendelezo wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 huko nchini Qatar, timu ya taifa ya Saudia Arabia imeonyesha maajabu baada ya kuishangaza Argentina kwa kuifunga mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi C uliopigwa katika dimba la Lusail mjini Doha.


Licha ya kuundwa na Wachezaji wakubwa duniani, wakiongozwa na Nahodha Lionel Messi, Angel Di Maria, Lautaro Martínez na wengine wengi, Argentina walianza kupata bao katika mchezo huo kwa mkwaju wa Penalti kupitia kwa Nahodha Messi dakika ya 10’ ya mchezo huo.

Kipindi cha kwanza kiliisha, Argentina wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Kikosi cha Kocha mwenye bahati kwenye mchezo wa Soka, Harvé Renard. Saudia Arabia walirudi kipindi cha pili wakiwa wanajua wanacheza na timu kubwa duniani.

Dakika ya 48’ Saudia walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Mshambuliaji, Saleh Al-Shehri, dakika ya 53’ waliwashangaza tena Argentina kwa kuongeza bao la pili kupitia kwa Winga wa timu hiyo, Salem Al-Dawsari na kufanya mabao hayo kudumu hadi dakika zote 90’ za mchezo.

Kundi C linaundwa na timu za Saudia Arabia wenye alama tatu, Argentina ambao hawana alama yoyote, Mexico na Poland ambao watacheza mchezo wao wa kwanza katika Kundi hilo.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments