UINGEREZA, MAREKANI VITA YAO YAISHA PATUPU…

 Mzunguko wa pili wa Kundi B la Michuano ya Kombe la Dunia 2022, umehitimishwa kwa timu za taifa za Uingereza na Marekani kutoshana nguvu bila kufungana (0-0) katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Al Bayt nchini Qatar.

Licha ya kushuhudiwa na Baba yake mzazi aliyekuwa jukwaani, Rais wa Liberia, George Weah Mshambuliaji wa Marekani, Timothy Weah ameshindwa kufurukuta katika mchezo huo akiwekwa chini ya ulinzi mkali na kina Harry Maguire, Luke Shaw, Kieran Trippier na John Stones.

Washambuliaji Marcos Rashford, Harry Kane, Bukayo Saka na kina Raheem Sterling wameshindwa kuwika mbele ya ukuta mgumu wa Marekani ulikuwa chini ya kina Walker Zimmerman, Sergino Dest na Antonee Robinson.

Baada ya sare hiyo, timu hizo zinajiweka nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata ya 16 Bora ya Michuano hiyo, ambapo Uingereza ndio wanajiweza pazuri kufuzu hatua hiyo ya mtoano.

Katika msimamo wa Kundi hilo B, Uingereza anaongoza akiwa na alama nne akishinda mchezo mmoja na kupata sare moja, nafasi ya pili ni Iran wenye alama tatu wakiwa tayari wamepoteza mchezo mmoja, huku Marekani wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa na alama zao mbili, wakiwa tayari wamepata sare katika michezo yote miwili.

Timu ya taifa ya Wales, wapo nafasi ya nne na ya mwisho katika msimamo huo wakiwa na alama moja pekee, wakiwa wamepata sare mchezo mmoja pekee na kufungwa mchezo mmoja.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments