UVCCM Geita Wajipanga Kumsaidia Rais Samia

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Geita wamejidhatiti kumusaidia Rais Samia Suluhu kutekeleza, kusimamia na kukamilisha miradi ya maendeleo kama ilivyopangwa na serikali.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita, Manjale Magambo wakati akizungumuza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika uchaguzi.

Manjale amebainisha miongoni mwa miradi hiyo ni mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Viktoria ambao tayari Rais Samia ameshatoa fedha na hivo UVCCM wamejipanga kushiriki mradi ukamilike kikamirifu.

Aidha mwenyekiti wa UVCCM ameahidi kushirikiana na viongozi wengine ndani ya mkoa ili kutekeleza maelekezo ya irani ya chama kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mikopo ya halmashauri.

“Nitaweza kukaa na hizi halmashauri zetu, tuangalie fursa ambazo zinapatikana katika kila wilaya tuweze kuamusha uzalishaji, kwa mfano kwa mkoa wetu wa Geita hasa zaidi ni uvuvi na uchimbaji wa madini.”

Manjale amewaomba vijana kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza wajibu wao ili kusaidia serikali ya awamu ya sita iweze kufanikisha sera za maendeleo kwa ufanisi kupitia hamasa na nguvu kazi imara.

Awali akitangaza matokeo ya uchanguzi wa UVCCM mkoa wa Geita, msimamizi mkuu wa uchaguzi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Hassan Masala aliwaomba vijana kushikamana.

Alimtaja Manjale kuwa mshindi wa kiti cha uenyekiti kwa kura 380 kati ya kura 415 zilizopigwa akifuatiwa nia Richard Jaba aliyepata kura 29, Sopspeter Bulugu kura tatu na Anisia Kajole kura moja

Chanzo Msumba News

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments