WAFANYAKAZI WIZARA YA NISHATI WAMETAKIWA KUTOJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA

      Wajumbe  wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara  ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja mkoani  Singida baada ya kumalizika kwa mkutano kwa njia ya mtandao uliohutubiwa na Waziri  wa wizara hiyo January Makamba jana.

Washiri wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Mkutano ukiendelea. 


WATENDAJI katika Wizara ya Nishati watakiwa kufanyakazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya Rushwa kama hatua ya kuongeza uaminifu kwa wananchi wanao watumikia.

Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Nishhati January  Makamba wakati akihutubia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa njia ya Mtandao unaofanyika mjini Singida.

Amesisitiza kuwa ubunifu na uwajibikaji mahali pa kazi ni jambo la msingi ili kuendelea kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi Mijini na Vijijini.

Makamba alisema  wizara hiyo itaendelea kusimamia na kutelekeza miradi ya kimkakati ukiwemo mradi mkubwa wa kufua umeme JNHPP ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 77.

Katika hatua nyingine amesema suala la kufikisha umeme wa gridi ya Taifa mkoani Kigoma ni jambo la kupongezwa ambapo kwa sasa Serikali imepata fedha za kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Kakono na miradi mingine ya kimkakati.

Waziri Makamba ameipongeza Menejimenti ya Wizara ya Wishati na Kamati zilizofanikisha maandalizi ya mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na kusema kuwa hicho ni kiashiria kizuri cha ushirikishwaji na uimarishwaji wa mahusiano mazuri kati ya menejimenti na wafanyakazi, hatimaye kutambua mchango wa kila mfanyakazi katika eneo lake la utumishi.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana imani kubwa na Watendaji pamoja na Viongozi wa Wizara ya Nishati, hivyo watumishi hawana budi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuendelea kuienzi imani hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amemhakikishia Waziri wa Nishati kuwa wataendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata kanuni ,taratibu na miongozo ili kuhakikisha Wizara inaendelea kutoa mchango mkubwa katika kukuza Pato la Taifa.

Na lsmail Luhamba,  Singida 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments