WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MAJI KISARAWE, AITAKA DAWASA KUHAKIKISHA WANAPELEKA MAJI KWA WANANCHI

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa maji wa Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Waziri Mkuu amesema kutokana na mvua zinazonyesha amepewa taarifa kuwa hali ya mto wa Ruvu inaridhisha hivyo wananchi wa Pwani pamoja na Dar es Salaam wanapata maji na hakuna mgao wa maji tena.

Amesema kutokana na upatikanaji wa maji ikijikumuhisha mradi wa maji wa Kisarawe itaongeza chachu kwa wananchi wa Kisarawe na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Dar es Salaam kupata maji ya uhakika kupitia mradi huo.

Pia amewataka DAWASA kuhakikisha vijiji vyote ambavyo havijapata maji kuhakikisha vinapata maji na kama kuna changamoto ya upatikanaji wa fedha basi ni jukumu la Serikali sasa kuhakikisha upatikanaji wa fedha ili kuweza kutanua wigo wa upatikani wa maji katika vijiji ambavyo bado kuna shida ya maji 

Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo kuhakikisha wanafanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji pamoja na Mazingira yanayozunguka vyanzo hivyo vya maji kwani kumekuwepo na ukaukaji wa vyanzo vya maji kutokana na uharibifu wa Mazingira.

Naye Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo amesema katika wilaya ya Kisarawe kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji lakini kutokana na mradi wa maji wa Kisarawe umeweza kupunguza kwa asilimia kubwa ya upatikanaji wa maji na hivyo anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha kwa ajili ya miradi ya maji katika wilaya hiyo.

Jafo ameiomba DAWASA kufikisha maji katika kata  ya  Masaki, Kiguta, Chang'ombe ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa asilimia kubwa katika wilaya ya Kisarawe hii ikiwa kufikia malengo ya kumtua mama ndoo kichwani.

Akitoa maelezo ya mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Kisarawe umejengwa kwa fedha za ndani Bilion 10.6 zilizotokana na makusanyo ya maduhuli ya mauzo ya maji.

Luhemeja amesema wakati wa utekelezaji wa mradi huo, DAWASA iliona fursa ya kujenga mradi mwingine wa Bilionj 7.3 wa kuyatoa maji katika tenki la Kisarawe linalohifadhi maji Lita Milioni 6 kupeleka katika maeneo ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa maji wa Kisarawe uliotekelezwa na DAWASA wakati wa ziara ya Waziri Mkuu ya kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza mara baada ya kupata maelezo ya mradi wa maji wa Kisarawe kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ha Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu namna maji yalivyowafikia wananchi mbalimbali kupitia mradi wa maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu maji hayo kiwafikia wananchi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Dar es Salaam alipomaliza kukagua Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita Milioni 6 katika mradi wa Maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiangalia ujazo wa maji kwenye Tanki la kuhifadhia majilenye ujazo wa Lita Milioni 6  katika mradi wa Maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akikagua mradi wa maji wa Kisarawe alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, wa pili kushoto ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiendeleq na ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa DAWASA pamoja na Wananchi waliofika kwenye mradi wa maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, wa kwanza kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Selemani Jafo akitoa maelezo kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Kisarawe kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa(wa pili kushoto) alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe uliotekelezwa na DAWASA wakati wa ziara katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Baadhi ya wafanyakazi wa DAWASA, viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  alipokuwa anazungumza alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyopo katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili kwenye mradi wa maji wa Kisarawe wakatiwa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa kwenye picha ya pamojwafamu na wakurugenzi na wafanyakazi wa DAWASA mara baada ya kumalizika kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe uliopo katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Picha ya pamoja

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments