ZELOTHE AREJEA KWA KISHINDO CCM ARUSHA

 

Zelothe Stephen  ametetea nafasi yake kwa kishindo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha,Zelothe ameshinda kwa kupata kura 683 kati ya kura  970  zilizopigwa katika nafasi ya Mwenyekiti.

Uchaguzi huo umefanyika  kwenye ukumbi wa Ukumbi wa Arusha International Conference Centre AICC ambapo kwa upande wa Mpinzani wa Mwenyekiti huyo ambaye ni Robert Kaseko alipata kura  281 kati ya kura hizo  zilizopigwa na hakuna kura zilizoharibika.

Ni katika uchaguzi uliofanyika jana ambapo amewashinda wapinzani wake wawili.

Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda amepongeza namna ambayo zoezi hilo la uchaguzi lilivyofanyika kwani lilikuwa la utulivu, amani kubwa kutokana hakukuwa na dalili zozote zenye kupelekea vurugu au vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo aliyechaguliwa katika uchaguzi huo “Mimi niwashukuru Sanaa ndugu Wajumbe kwa hili kubwa mlilolifanya la kunipa dhamana hii kubwa naomba tu ushirikiano wenu ili tuzidi kulisukuma mbele gurudumu hili la maendeleo kupitia Jumuiya ya Wazazi”,


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments