Benki Ya NBC Yamkabidhi Fiston Mayele Tuzo Kama Mchezaji Bora Mwezi Novemba

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Tsh milioni 1 pamoja na tuzo kwa mchezaji wa Yanga Fiston Mayele alietangazwa mchezaji bora wa ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa mwezi wa November . Anayeshuhudia kulia ni Mjumbe Bodi ya Ligi Bw.Bw. Azim Khan mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Young Africans SC dhidi ya Coastal Union uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa mapema jana .[/caption]   Dar es Salaam: Disemba 21 , 2022: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premier League jana ilikabidhi zawadi ya pesa na tuzo kwa mchezaji bora wa ligi hiyo wa mwezi November , Fiston Mayele kutoka klabu ya Yanga. Makabidhiano ya zawadi hizo yalifanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya Yanga SC dhidi ya Coastal Union uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo ambao ulikamilika kwa timu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 3 kwa sifuri. Magoli ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Fiston Mayele alifunga magoli mawili na Feisal Salum alifunga goli 1 na Katika tukio la makabidhiano ya zawadi hizo, ilishuhudiwa na mjumbe wa bodi ya ligi Bw. Azim Khan ambapo Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru alikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya Tsh milioni 1 kwa mchezaji huyo wa Yanga Fiston Mayele pamoja na tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi Novemba. Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru amesema NBC itaendelea kutoa hamasa kwa wachezaji na makocha kwa kila mwezi ili kuleta ushindani kwa wachezaji na makocha wote wanaoshiriki Ligi kuu.    “Tuzo hizi za kila mwezi tunazitoa kwa kuleta hamasa kwa wachezaji na makocha wa kila timu zinazoshiriki Ligi kuu ili wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa ,pia kusaidia kuboresha mchezo huu wa soka hapa nchini”amesema Nduguru Pia akifafanua zaidi mipango ya Benki hiyo kuboresha Udhamini wake ambapo wapo katika hatua za mwisho kuanza kutoa mikopo ya mabasi kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi kuu kurahisisha usafiri wa vilabu hivyo. “Pia NBC tunaendelea kudhamini michezo mingine zaidi hapa nchini kama riadha kupitia NBC Dodoma Marathon na mashindano ya mchezo wa Golf tukidhamini klabu ya Lugalo , lengo letu ni kusaidia sekta ya michezo nchini kuwa na kiwango cha kimataifa na pia kuboresha maslahi ya wanamichezo kwa ujumla.“ Kwa upande wake Mchezaji wa Yanga Fiston Mayele alishukuru kupata tuzo hiyo na kuahidi kuwa atazidi kuongeza bidii kuwa kinara katika timu yake na kusaidia timu yake kupta ushindi wa kila mechi. “Napenda kuwashukuru NBC kwa kutoa tuzo hii inaongeza sana hamasa upande wangu na wa wachezaji wote na makocha,pia nawashukuru benchi la ufundi na wachezaji wenzangu kwa pamoja wameniwezesha kupata tuzo hii na nitazidi kufanya vizuri.   Mwisho.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments