FEISAL AAGA YANGA SC, WENYEWE WADAI BADO NI WAO…

 Kiungo Feisal Salum Abdallah (Feitoto) rasmi amewaaga waajiri wake wa zamani Young Africans SC wakati huu akihusishwa zaidi kutimkia Azam FC, usajili uliotajwa kukamilishwa katika dirisha dogo lililofunguliwa kuanzia Desemba 15, 2022 hadi Januari 15 mwaka 2023.

Kupitia taarifa hiyo ya kuwaaga Wananchi, Feitoto amesema maisha huja na kupita, huku akieleza kuwa kuna wakati maisha hayo yanajirudia, Feisal amesema atakumbuka yote mazuri yaliyotokea wakati akiitumikia Klabu hiyo, na kusahau yote mabaya.

“Umekuwa wakati mzuri sana kucheza Young Africans SC, Klabu yenye historia kubwa na ya kuvutia nchini na Afrika yote”, ameeleza Fetoto a.k.a Fahlasuhfi 

Hata hivyo, Waajiri wake wa zamani, Yanga SC wamedai kuwa Feisal ni Mchezaji halali wa timu hiyo na tayari walimuagiza Mchezaji huyo kuzingatia matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo. 

“Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo tarehe 30 Mei 2024”.

Aidha, Yanga SC wanedai kutejesha fedha kiasi cha Tsh. 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu hiyo.

“Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans”, imeeleza taarifa ya Yanga SC.

Feisal Salum alijiunga Yanga SC akitokea katika Klabu ya JKU ya nyumbani kwao Zanzibar mwaka 2018, baada ya kutangazwa kuwa Mchezaji wa Singida United asubuhi - jioni Yanga SC ilimtangaza Kiungo huyo kuwa Mchezaji wao huru.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments