GEITA GOLD FC YAMUACHA MPOLE


  
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Klabu ya Soka ya Geita Gold imetangaza kuachana na Mshambuliaji George Enock Mpole ambaye msimu uliopita alikuwa kinara wa mabao katika timu hiyo yenye maskani yake mjini Geita.

Taarifa za Geita Gold FC kuachana na Mpole zimethibitishwa na Mtendaji Msaidizi wa Klabu hiyo, ambapo Mshambuliaji huyo ameruhusiwa kucheza timu yoyote kutokana na kufika kikomo kwa mkataba wake katika Klabu hiyo, mnamo Desemba 7, 2022.

“Uongozi wa Klabu ya Geita Gold unakutaarifu rasmi ya kwamba mkataba wako wa ajira kati ya Klabu na wewe umemalizika rasmi leo baada ya pande zote mbili kukubaliana na uko huru kujiunga na Klabu yoyote kuanzia leo”, ameeleza Mtendaji Msaidizi kupitia taarifa iliyoandaliwa ya kuachana na Mshambuliaji huyo.

Geita Gold FC imemshukuru Mshambuliaji huyo kwa ushirikiano wake na kazi nzuri tangu asajiliwe ndani ya Klabu, pia Klabu hiyo imemtakia kila la kheri na maisha mema katika majukumu yake ya Soka katika Klabu nyingine.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments