Halmashauri itakayopata kipindupindu Mbeya, viongozi kuwajibishwa

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameziagiza halmashauri zote mkoani humo kuzingatia usafi wa mazingira ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika msimu huu wa mvua na eneo ambalo ugonjwa huo utalipuka, viongozi watawajibishwa.

Homera ametoa agizo hilo  leo Jumamosi Desemba 31,2023  wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa ikiwa ni siku ya usafi wa mazingira wa mwisho wa mwezi huku akisisitiza jiji limekuwa katika hali mbaya ya uchafu.

“Naagiza maofisa afya, wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuhakikisha kila eneo linakuwa safi vinginevyo atachukua hatua kwa ambaye eneo lake litakuwa chafu au kuibuka kwa kipindupindu.” amesema Homera

Mwenyekiti wa wafanyabiashara soko la Sido, Huruma Nsangalufu amesema kuondolewa kwa maguba katika soko hilo kumechangia ongezeko la uchafu na wafanyabishara kuwa hatarini kuugua magonjwa ya matumbo kutokana na mazalio ya nzi.

“Nishauri jiji katika maeneo ya masoko warejesha mfumo wa maguba kwani kwa sasa hali ni mbaya zaidi taka zinatupwa kiholela ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya hatari kutokea,” alisema Dk Tulia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments