KIWANGO CHA MAAMBUKIZI MKOANI PWANI KIMESHUKA , WANANCHI WAASWA KUENDELEA KUPIMA AFYA ZAO

 Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na Vifo vitokanavyo na ugonjwa huo ,mkoani Pwani kimeshuka kutoka asilimia 5.9 hadi kufikia asilimia 5.5.

Akitoa hali ya kiwango Cha maambuzi ya ugonjwa huo, katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani Mkoani Pwani yaliyofanyika viwanja vya shule ya msingi Mtongani, Kibaha ,mwakilishi wa mkuu wa mkoa huo ,mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri, alieleza kiwango hicho kimeshuka kati ya kipindi cha mwaka 2012 hadi 2017.

Alieleza ,mbali ya mafanikio hayo Halmashauri ya Kibaha Mjini , Mkuranga na Chalinze bado zina maambukizi makubwa kutokana na changamoto ya muingiliano wa idadi ya watu wanaotoka nje ya halmashauri hizo.

Aidha ,Sara alieleza kundi la vijana pamoja na wanaume wanaonekana kuwa na mwamko mdogo wa kujitokeza kupima afya zao.

Alifafanua , katika kipindi cha mwezi January Hadi Novemba mwaka huu takwimu zinaonyesha ,kuna maambukizi mapya ya vijana 1,004 wenye umri kati ya miaka 15-24 .

"Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni IMARISHA USAWA, Lazima tuweke usawa ,unaweza kuona vijana hawa ni wadogo ,Lakini tukumbuke umri huu ni wa kukua ,na ndio wanaojiingiza katika maadili yasiyo mema ikiwemo madada poa,wavuta bangi na madawa ya kulevya hivyo kujikuta wakipata maambukizi ya virusi hivyo"alisema Sara.

Awali muathirika wa VVU kutoka kata ya Kikongo, Elizabeth Ngonyani alieleza ,kuugua Ukimwi sio kufa kwani tangu agundulike kuwa na ugonjwa huo ,na wapo waliokufa na kumuacha yeye akiwa afya njema.

Nae dkt. Sisty Moshi kutoka THPS alieleza ,THPS inafadhiliwa na Serikali ya Marekani na inashirikiana na mkoa huo kwa miaka kumi Sasa .

Alisema kiwango Cha upimaji mkoa upo kiwango Cha asilimia 95 na walio kwenye dawa za kufubaza VVU ni takriban watu 50,000 sawa na asilimia 98.

Moshi alieleza, kwa mwaka huu wametoa fedha Bilioni 3.2 kwa ajili ya shughuli za Halmashauri .

Kaimu Katibu Tawala mkoani Pwani,Rukia Mhango aliishukuru THPS ,AMREF na wadau wengine wa jamii kwa kuboresha Mazingira ya utoaji huduma za kiafya .

Aliwaasa ambao wamegundulika na VVU na kuanza dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi wasiache dawa na wasiwe watoro kufuata dawa na kuhudhuria kliniki zao.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments