Makaburi 1,500 kuhamishwa kupisha ujenzi SGR

 Makaburi takribani 1,500 ya Waislamu yaliyoko Mtaa wa Sokoni Mkuyuni jijini Mwanza yameanza kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga na kupelekwa katika makaburi ya Nyashana kata ya Isamilo jijini humo.

 Mchakato wa uhamishaji wa makabuli hayo ulianza Desemba 18, 2022 na kutarajiwa kuhitimishwa makaburi hayo yatakapoondolewa yote ambapo hadi kufikia leo Desemba 23 mwaka huu mabaki ya miili 198 ilikuwa imeshafukuliwa na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Nyashana jijini Mwanza.

Rehema Haroun ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu aliyezikwa katika makaburi hayo, ameeleza kuridhishwa na ufukuaji wa miili ya wapendwa wao huku akiziomba mamlaka kuendelea kuongeza umakini ili kuepusha mkanganyiko wa utambuzi wa miili hiyo.

Rehema ametaja changamoto iliyoibuka katika shughuli hiyo kuwa ni pamoja na watu zaidi ya watatu kudai waliwazika wapendwa wao katika eneo lenye kaburi moja.Rehema Haroun ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu aliyezikwa katika makaburi hayo, ameeleza kuridhishwa na ufukuaji wa miili ya wapendwa wao huku akiziomba mamlaka kuendelea kuongeza umakini ili kuepusha mkanganyiko wa utambuzi wa miili hiyo.

Rehema ametaja changamoto iliyoibuka katika shughuli hiyo kuwa ni pamoja na watu zaidi ya watatu kudai waliwazika wapendwa wao katika eneo lenye kaburi moja.


Mhandisi Mwita amesema kila mwenye ndugu aliyezikwa hapo atalipwa Sh300,000 kama kifuta machozi baada ya shughuli ya kuyaamisha kukamilika huku akisisitiza kuwa fedha hiyo itaongezeka endapo kaburi lilikuwa limeboreshwa ikiwemo kujengewa vigae.

"Haturuhu wafiwa kufika hapa kwani itaibua kilio bali tunahitaji wawakilishi wa familia ambao watashuhudia mabaki ya wapendwa wao yakiondolewa lengo ni kuhakikisha utaratibu unafuatwa, baada ya kukamilisha kuyahamisha tutapeleka majina ya waliokutwa hapa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili kulipwa kifuta machozi," amesema mhandisi huyo

Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sophia Kiluvia amesema shughuli ya kuhamisha mabaki ya miili ya watu waliozikwa katika eneo hilo inafanyika kitaalam ili kuhakikisha hakuna mwili utakaosalia katika eneo hilo.

Pia amesema wanazingatia taratibu zote za kuanzia kuchimba kabuli, utambuzi wa miili iliyozikwa katika eneo la kabuli husika, kusafirishwa hadi makabuli ya Nyashana na kuzikwa kwa mara nyingine.

"Tupo hapa kuhakikisha taratibu zote za kiafya zinazingatiwa, wanaofukua hawapati madhara kiafya, ndugu wa marehemu wanakuwa salama hata wakazi wa eneo hili hawaathiriki na shughuli hii, tunazidi kuomba watu wenye ndugu waliozikwa hapa waendelee kujitokeza," amesema Sophia

Naye, Mwakilishi wa Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata) wilaya ya Nyamagana, Juma Malijani amesema eneo hilo lililoanza kutumiwa na Waislamu miaka 76 iliyopita, lilikuwa likitumiwa na waumini wa Kiislamu kutoka Msikiti wa Lukumani, Johari, Ghazari na Shede iliyoko katika kaya hiyo.


Pia, amewataka watu wenye ndugu waliozikwa katika eneo hilo kitotumia shughuli hiyo kama kitega uchumi na kusema hakuna fedha inayoweza kuthaminishwa na binadamu hivyo akawataka kujitokeza kwa wingi.

"Natambua kuwa wapo watu ambao wanasita kuja kushuhudia mabakinya ndugu zao yakiondolewa wakishinikiza kuongezewa hela, niseme tu hii siyo fidia bali ni kifuta machozi kwani hakuna pesa inayoweza kuthaminishwa na binadamu, tujitokeze kuwapumzisha ndugu zetu," amesema Malijani ambaye pia ni Shehe.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments