MBUNGE SINGIDA MJINI ATOA MILIONI 5 KUCHANGIA UJENZI WA ZAHANATI

 

 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mwalimu Mussa Sima (katikati) akiwa katika picha na Wazee baada ya kufanya kikao na baraza la wazeewa Kata ya Unyianga katika ziara yake aliyoifanya juzi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Na Dotto Mwaibale, Singida. 

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mwalimu Mussa Sima ametoa Sh. Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Unyianga iliyopo Manispaa ya Singida ambapo Serikali ilitoka Sh. 50 Milioni.

Ujenzi wa Zahanati hiyo umekwisha kamilika na tayari watumishi wawili wamekwisha fika ambao ni daktari na muuguzi.

Akizungumza wakati wa ziara yake aliyoifanya juzi Desemba 20, 2022 ya kukagua miradi ya maendeleo Sima alisema Serikali umefanywa kazi kubwa katika jimbo kwa kutoa Fedha nyingi.

Miradi aliyoitembelea na kuikagua ni ujenzi wa Shule ya Sekondari katika kata hiyo, ujenzi wa madarasa mawili shule ya Msingi ambapo alichangia Sh. 2 Milioni na kukagua ujenzi wa barabara za Kindai-Unyianga inayojengwa sambamba na madaraja na kunyanyua tuta barabara ya Unyianga Mwankoko.

Alisema barabara hiyo imekamilika baada ya  Serikali Kuu kutoa Sh.370 Milioni fedha ambazo zimechagiza kuchochomea kasi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Katika hatua nyingine Mbunge Sima alipata fursa ya kuzungumza na baraza la wa wazee wa kata hiyo sanjari na kula nao chakula.

Aisha Sima alizungumza na makundi ya wauza kahawa na vikundi vya akina mama na kukiunga mkono kwa kukipa Sh   120, 000 na  kikundi cha wauza kahawa  Sh 70, 000 na kuwapongeza kwa umoja wao.

Katika ziara hiyo Mbunge Sima aliongozana na Diwani wa Kata ya Unyianga,  Geofrey  Mdama ambapo alitumia nafasi hiyokumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo.

Mbunge Sima akitoa mchango kuwaunga mkono wauzaji wa Kahawa wakati wa ziara hiyo.
Mbunge Sima akibadilishana mawazo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Unyianga wakati wa ziara hiyo. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments