MOROCCO YAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

 Timu ya taifa ya Morocco imekuwa timu pekee kutoka bara la Afrika kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, baada ya ushindi wa jumla wa changamoto ya mikwaju ya Penalti 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Hispania katika dimba la Education City.Licha ya kupiga mpira mwingiii katika mchezo huo na kupiga ‘pasi’ zaidi ya 1000, Hispania walishindwa kuifungua ngome ya Morocco iliyokuwa bora wakati wote wa dakika 120’ za mchezo huo wa hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo, hivyo hadi dakika hizo zinaisha timu hizo zilitoka sare ya 0-0.

Hata hivyo, katika mikwaju ya Penalti, Hispania hawakupata mkwaju hata mmoja kutokana na ubora wa Golikipa wa Klabu ya Sevilla, Yassine Bounou ambaye aliyekuwa katika lango la Morocco katika changamoto hiyo ya mikwaju ya Penalti.

Mkwaju wa tatu wa Kiungo wa Hispania, Sergio Busquets uliizamisha Hispania katika mchezo huo, mkwaju huo ulipanguliwa na Golikipa Bounou, mkwaju wa mwisho wa Morocco uliopigwa na Mlinzi wa pembeni wa timu hiyo Achraf Hakimi uliivusha Morocco katika hatua hiyo ya Robo Fainali.

Morocco watasubiri mshindi katika ya Ureno dhidi ya Switzerland, ili kukabiliana nao katika hatua ya Robo Fainali, mchezo huo kati ya Ureno dhidi ya Switzerland utakuwa wa mwisho wa hatua hiyo ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments