ONYO KALI YATOLEWA NA JESHI LA POLISI KAGERA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWAKA

 

Jeshi la polisi mkoani Kagera limetoa onyo na tahadhari kali kwa mtu au kundi la watu wenye lengo la kufanya vitendo vya kiharifu kutojihusisha na matendo maovu.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa polisi Mkoa Kagera William Mwampaghale wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kamanda Mwampaghale amesema kuwa inapofika wakati wa sikukuu mambo mengi hujitokeza yakiwemo ya kiharifu hivyo kutokana na jeshi hilo kujipanga ki sawa sawa hategemei kuona matendo maovu yakijitokeza huku akionya wale wote wenye nia ya kuhatarisha usalama kuwa hawana nafasi.

"Katika kuelekea siku kuu za Krisms na Shamrashamra za kupokea mwaka mpya,nitoe onyo kwa wote wataojihusisha na uchomaji wa matairi barabarani wakati wa sherehe hizo,tabia pia ya kuendesha magari kwa kasi barabarani haitaruhusiwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao pia tabia ya ulevi wa kupindukia na kulewa kisha kuendesha vyombo vya moto haitavumiliwa alisema" kamanda Mwampaghale.

Kamanda huyo pia amepiga marufuku suala la disco toto huku akiwataka wananchi kuacha tabia za kurundikana katika kumbi maarafu ili kujiepusha na madhara yatokanayo na msongamano na kuwa kwa wale watakao penda kusherekea mwaka mpya kwa kufyatua fataki wafuate utaratibu na vibali kutoka katika jeshi hilo vinginevyo watakao kiuka hatua za sheria zitachukuliwa dhidi yao.

Ameongeza kuwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika msimu huu wa kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka za Chrismas na mwaka mpya vimejipanga kuhakikisha kuwa waumini na wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kwa ujumla kabla,wakati na baada ya sherehe hizo wanasherekea kwa amani na utulivu.

Aidha amesema kuwa jeshi hilo limejiimarisha vyema katika kuhakikisha mifumo ya kuzuia vitendo vya kiharifu inasimama vizuri ikiwa ni pamoja na askari wa doria za magari, pikipiki, doria za miguu, doria za mbwa na farasi pamoja na doria za boti majini.

Jeshi hilo limewaomba wananchi kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyoweza kupelelekea uvunjifu wa amani na kutii sheria bila shuruti badala yake watoe ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha hali ya usalama,utulivu na amani wakati wote na hata baada ya sikukuu hizo za mwisho wa mwaka huku akiwahimiza wananchi kuchukua tahadhari watakapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu.
Na Shemsa Mussa, Kagera.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments