RAIS SAMIA AMWAGA MAMILIONI KWA WASANII

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa ametoa hundi za mamilioni ya fedha kwa wadau waliokidhi kukopa kwenye mfuko wa Utamaduni na Sanaa na amewataka wasanii na wadau wa kazi za sanaa kujitokeza kwa wingi kuomba kukopeshwa fedha kutoka kwenye mfuko huo alioufufua Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.Mfuko huo haukuwepo tangu mwaka 2013 ulipositishwa ule wa awali.

Mhe.Mchengerwa amesema haya Disemba 23, 2022 jijini Dar es Salaam akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kwenye uzinduzi rasmi wa utoaji mikopo kutoka kwenye mfuko huo ambapo uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa Sanaa na Utamaduni.

Aidha, wakati wa uzinduzi huo wadau wa tano kati ya kumi na tisa waliowasilisha maombi yao walipatiwa fedha za mfuko huo.

Jumla ya shilingi milioni 170 zimetolewa katika mkupuo wa kwanza ambapo msanii wa chini amepata shilingi milioni 20 na wa juu amekopeshwa kiasi cha shilingi milioni 50. Utoaji wa mikopo hiyo ndio kwanza umeanza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments