RAIS SAMIA ARIDHIA KUFUFULIWA KWA MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI BONDE LA BUGWEMA MUSOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kuendeleza mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Bugwema lililopo Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo wakati wa ziara ya kutembelea eneo hilo akiwa na Viongozi kadhaa wa Musoma Vijijini walioambatana na Timu ya Wataalamu. 

 kuwa, Rais aliridhia suala hilo 
"Mhe Rais Samia, alipotembelea Musoma Vijijini Februari 6, mwaka huu akizindua Mradi wa ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango- Kiabakari- Butiama, aliridhia ombi la kuendeleza mradi huu mkubwa wa umwagiliaji 

"Katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma, tarehe 7-8.12.2022 niliwasilisha tena ombi hili na jana 29.12.2022, Timu ya Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilitembelea Bonde la Bugwema, Timu hiyo iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Raymond Mndolwa."alisema Mbunge huyo.

Aidha, aliongeza kuwa: Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikusudia kuanzisha kilimo kikubwa cha umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema.

Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.

"Bonde la Bugwena ni kubwa, eneo lililokusudiwa kulimwa wakati huo ilikuwa ni ndani ya hekta 10,000.

Bonde lenyewe likichukuliwa kwa ujumla wake lina ukubwa wa zaidi ya hekta 20,000." Alisema Mh Prof. Muhongo.

Aidha amebainisha kuwa, Miundombinu ya umwagiliaji ilijengwa miaka hiyo, lakini utekelezaji wake ukasimama.

Mazao makuu yanayolimwa ndani ya Bonde hilo ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu na pamba.

"Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kwamba matayarisho ya utekelezaji wa Mradi wa Bugwema yanaendelea vizuri kwa ajili ya kuanza kufanya "feasibility studies and designs".

"Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani nyingi sana kwa Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuendeleza Mradi wa Kilimo kikubwa cha Umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema.

Upatikanaji wa chakula kingi cha bei nafuu kunasaidia kushusha mfumuko wa bei kwenye soko la chakula" alisema Prof. Muhongo Chanzo Michuzi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments