SERIKALI BABATI YAMALIZANA NA MADEREVA BAJAJI

Madereva bajaji Mjini Babati wanaotumia Kituo Cha sheli ya Meru Kona ya Mrara  wameandamana hadi ofisi za Chama cha Mapinduzi kushinikiza kuachwa Kwenye eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema eneo wanalolitumia madereva bajaji hao lipo sehemu hatarishi kwa kuwa ni jirani na kituo Cha mafuta.
Twange amewataka madereva hao wakae wenyewe kutatua mgogoro huo ambao umeanza tangu mwaka Jana.

Amesema madereva hao hawahushimu makubaliano ndo maana mgogoro unaendelea.
"Tunasaidieni sisi tunao watetea kwa sababu huu wema unafika mwisho" alisema Twange.
Mwenyekiti wa Bajaji Mjini Babati Lomboi Osisia amesema wamelitumia eneo hilo muda mrefu kama kituo chao cha kusubiria abiria.

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Anna Fissoo amesema changamoto ya bajaji wameshaitatua kwa kuwahamishia kwenye kituo Cha msikitini kona ya Mrara.
Mkuu wa Usalama barabarani mkoa wa Manyara Georgina Matagi amewataka madereva kuheshimu taratibu za Usalama barabarani na usafirishaji  zinavyoelekeza na kwamba wataendelea kusimamia sheria na taratibu zote.

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi mjini Babati Elizabeth Marley amewataka madereva hao wawe watulivu na kuendelea na kazi zao kwani Serikali ya CCM ni sikivu.

Na John Walter-Manyara

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments