SERIKALI imeunda kamati ya kutanzua mgogoro wa mipaka ya ardhi baina ya wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Bonde la Wembere unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilayani Iramba mkoani Singida, uliodumu kwa muda wa miaka mitatu. Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mary Masanja, alipotembelea eneo hilo lenye mgogoro, akiambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi. Ziara ya Mawaziri hao wawili katika Hifadhi ya Msitu wa Bonde la Wembere yenye ukubwa wa zaidi ya hekta za mraba elfu 54, unafuatia malalamiko ya wakazi wa eneo hilo ambao wamezuiwa kufanya shughuli zozote za kuwawezesha kujikimu kimaisha kwa vile wako ndani ya hifadhi. Mheshimiwa Masanja alisema kuwa Serikali inataka kuona mgogoro huo unamalizika na kuitaka kamati hiyo iliyoundwakushughulikia mgogoro huo inakamilisha kazi hiyo kwa wakati kwa kuzishirikisha kikamilifu pande zote zinazohusika ili kupata suluhu ya kudumu. Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo imepewa jukumu la kupitia upya mipaka iliyowekwa na TSF na kulalamikiwa na wananchi wanaoendesha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi katika eneo hilo zikiwemo shughuli za uvuvi, kilimo na ufugaji. Aidha, Mheshimiwa Mary Masanja, aliuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya hiyo ya Iramba, kuwarejeshea wananchi mali zao walizozikamata na kuzishikilia ikiwemo, pikipiki na majembe ili kuendeleza hali ya utulivu na amani iliyopo katika eneo hilo. Hata hivyo, Naibu Waziri huyo wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja, alikemea kitendo cha baadhi ya wananchi walioharibu miundombinu ya Mradi wa uoteshaji wa kitalu chkijiji cha Ujungu kata ya Mtekente, ikiwemo kuvunja uzio na kuharibu kisima cha maji na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 50. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb), wakiwasili katika Kijiji cha Msai kata ya Mtowa, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi wa eneo hilo na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaosimamia Hifadhi ya Msitu wa Bonde la Wengere. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na wananchi wa Kijiji Msai kata ya Mtowa, tarafa ya Shelui, Wilayani Iramba mkoani Singida, walipowasili na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani), kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi wa eneo hilo na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wanaosimamia Hifadhi ya Bonde la Wembere. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msai Kata ya Mtowa kuhusu namna Serikali ilivyodhamiria kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi na Hifadhi ya Bonde la Wembere, akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani). Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb), (kushoto), walipotembelea na kukagua eneo la Hifadhi ya Bonde la Wembere, lenye mgogoro baina ya wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaosimamia Hifadhi ya Msitu huo kuhusu mipaka.

 SERIKALI imeunda kamati ya kutanzua mgogoro wa mipaka ya ardhi baina ya wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Bonde la Wembere unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilayani Iramba mkoani Singida,  uliodumu kwa muda wa miaka mitatu.


Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mary Masanja, alipotembelea eneo hilo lenye mgogoro, akiambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Ziara ya Mawaziri hao wawili katika Hifadhi ya Msitu wa Bonde la Wembere yenye ukubwa wa zaidi ya hekta za mraba elfu 54, unafuatia malalamiko ya wakazi wa eneo hilo ambao wamezuiwa kufanya shughuli zozote za kuwawezesha kujikimu kimaisha kwa vile wako ndani ya hifadhi.

Mheshimiwa Masanja alisema kuwa Serikali inataka kuona mgogoro huo unamalizika na kuitaka kamati hiyo iliyoundwakushughulikia mgogoro huo  inakamilisha kazi hiyo kwa wakati kwa kuzishirikisha kikamilifu pande zote zinazohusika ili kupata suluhu ya kudumu.

Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo imepewa jukumu la kupitia upya mipaka iliyowekwa na TSF na kulalamikiwa na wananchi wanaoendesha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi katika eneo hilo zikiwemo shughuli za uvuvi, kilimo na ufugaji.

Aidha, Mheshimiwa Mary Masanja, aliuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya hiyo ya Iramba, kuwarejeshea wananchi mali zao walizozikamata  na kuzishikilia ikiwemo, pikipiki na majembe ili kuendeleza hali ya utulivu na amani iliyopo katika eneo hilo.

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja, alikemea kitendo cha baadhi ya wananchi walioharibu miundombinu ya Mradi wa uoteshaji wa kitalu chkijiji cha Ujungu kata ya Mtekente, ikiwemo kuvunja uzio na kuharibu kisima cha maji na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 50.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb), wakiwasili katika Kijiji cha Msai kata ya Mtowa, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi wa eneo hilo na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaosimamia Hifadhi ya Msitu wa Bonde la Wengere.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na wananchi wa Kijiji Msai kata ya Mtowa, tarafa ya Shelui, Wilayani Iramba mkoani Singida, walipowasili na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani), kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi wa eneo hilo na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wanaosimamia Hifadhi ya Bonde la Wembere.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msai Kata ya Mtowa kuhusu namna Serikali ilivyodhamiria kutatua mgogoro wa mipaka baina ya wananchi na Hifadhi ya Bonde la Wembere, akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb), (kushoto), walipotembelea na kukagua eneo la Hifadhi ya Bonde la Wembere, lenye mgogoro baina ya wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaosimamia Hifadhi ya Msitu huo kuhusu mipaka.  

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments