Serikali Yasitisha Uchimbaji Madini kijiji cha Nyabichune, Nyamongo.

Naibu Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa amesema katika operesheni ya awali iliyofanyika kijijini hapo hivi karibuni ilibainika kuwa jumla ya watu 10 wanafanya shughuli za uchimbaji katika makazi yao na kwamba kwa pamoja walizuiliwa kuendelea na shughuli hizo lakini imebainika kuwa wapo baadhi yao wamekaidi zuio  hilo na wanaendelea na uchimbaji.

Naibu Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa ameagiza kusimamishwa mara moja shughuli za uchimbaji wa madini kwenye makazi ya watu katika kijiji cha Nyabichune eneo la Nyamongo wilayani Tarime kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maisha ya watu.


Ametoa agizo hilo jana Desemba 5, 2022 alipofanya ziara kijijini hapo na kujionea namna baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wanavyofanya shughuli za uchimbaji kwenye makazi yao jambo ambalo mbali na kuwa linahatarisha maisha yao, ni kinyume cha sheria.

Kuanzia sasa nasitisha uchimbaji huu unaofanyika kienyeji katika kijiji hiki lakini pia kuanzia wiki ijayo wizara italeta wataalamu kufanya operesheni maalum kubaini wale wote wanaofanya uchimbaji hapa na hatua zichukuliwe,” amesema.


Amesema katika operesheni ya awali iliyofanyika kijijini hapo hivi karibuni ilibainika kuwa jumla ya watu 10 wanafanya shughuli za uchimbaji katika makazi yao na kwamba kwa pamoja walizuiliwa kuendelea na shughuli hizo lakini imebainika kuwa wapo baadhi yao wamekaidi zuio  hilo na wanaendelea na uchimbaji.


Kiruswa amesema licha ya uchimbaji huo kuhatarisha maisha ya watu, imebainika kuwa watu hao wanachimba katika eneo lenye leseni kubwa ya mwekezaji ambaye ni mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara, jambo ambalo pia ni kinyume cha utaratibu.


“Sisi hatuna nia ya kumnyayasa mtu yeyote lakini lazima sheria ifuatwe, kama tayari eneo lina leseni na amepewa mwekezaji lazima tusimamie sheria lakini kama mnakumbuka serikali tayari imetangaza kuwatambua wachimbaji wadogo na kinachofanyika ni kurasimisha shughuli zao. Sasa hatuwezi kurasimisha shughuli zenu kwenye eneo ambalo tayari kuna mtu ana leseni.”


“Mbaya zaidi uchimbaji unaofanyika hapa hauzingatii sheria za usalama na mazigira pia kuna mashimo mengine yameingia hadi mita 150 kwenye mgodi wa Barrick pia uchimbaji unafanyika chini ardhini wengine wamefika chini ya nyumba zao ina maana ikitokea Barrick amefanya ulipuaji mkubwa uwezekano wa hizi nyumba kuzama ni mkubwa,” amesema.


Naibu Waziri huyo amesema pamoja na mambo mengine suala la usalama wa raia na mali zao ni moja ya kipaumbele cha serikali na kwamba haiwezi kukubali aibu ya maafa yanayoweza kutokea katika kijiji hicho kutokana na uchimbji huo holela.


Meneja Mahusiano wa mgodi wa Barrick North Mara, Filbert Mworia amesema moja ya changamoto wanayokutana nayo katika eneo hilo ni baadhi ya watu kukataa kupokea fidia zao kwa madai kuwa malipo hayalingani na thamani ya mali zao.


“Hapa uthamini ulifanyika mwaka 2011 na asilimia 99 ya watu wamepokea malipo yao ila kuna watu 55 ambao wamegoma hadi leo lakini sisi tuko tayari kulipa na kuna cheki ya Sh1.8 bilioni ipo ofisini hadi sasa,” amesema Mworia.


Mmoja wa watu waliokutwa akichimba madini kwenye eneo hilo, Mwita Bwise amesema kuwa amemua kufanya hivyo ikiwa ni njia moja wapo ya kujipatia kipato

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments