SIMBA SC, YANGA SC KIBARUANI KIMATAIFA

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Soka barani Afrika, Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) tayari wamepangwa makundi ya Michuano hiyo msimu wa 2022-2023.

Katika droo hiyo iliyoendeshwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) mjini Cairo nchini Misri, Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wanaowakilisha taifa kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wamepangwa Kundi C na timu za Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea na Vipers SC ya Uganda.

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Young Africans Swamepangwa Kundi D na timu za TP Mazembe ya DR Congo, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali.

MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA (CAF CL)

Katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika; Kundi A lina timu za Wydad AC ya Morocco, Petro Luanda ya Angola, JS Kabylie ya Algeria na AS Vita Club ya DR Congo.


Kundi B lina timu za Al Ahly SC ya Misri, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal Club ya Sudan na Coton Sport ya Cameroon.

MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO (CAF CC) 
Michuano ya Kombe la Shirikisho; Kundi A lina timu za USM Alger ya Algeria, Marumo Gallants FC ya Afrika Kusini na FC Saint-Éloi Lupopo ya DR Congo.

Kundi B lina timu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, Rivers United ya Nigeria, CSMD Diables Noirs ya Congo Brazzaville na DC Motema Pembe ya DR Congo. Wakati Kundi C lina timu za Pyramids ya Misri, Future FC ya Misri, ASKO Kara FC ya Togo na AS FAR Rabat ya Morocco.

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia mwezi Februari, Machi hadi Aprili 2023 kwa timu zote kumenyana nyumbani na ugenini.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments