UVCCM BABATI MJINI WAFANYA USAFI HOSPITALI YA MRARA NA STENDI

Katika kuelekea siku kuu za chrismas na mwaka mpya, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Babati Mjini   wamefanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Mji Mrara na kwenye maeneo mbalimbali mjini hapo.

Mwenyekiti wa UVCCM Babati mjini Magdalena Urono amesema wameamua kumaliza mwaka 2022 kwa kufanya usafi kwenye maeneo hayo na kuhamasisha vijana kuendelea na utaratibu huo kwenye maeneo yao.

Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Maisaka amesema mbali na zoezi la usafi kupitia kampeni ya Safisha Kitaa, pia watatoa misaada mbalimbali kwenye vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Usafi uliofanyika ni kufyeka nyasi, vichaka na kuchoma taka zilizozagaa mitaani ili mji wa Babati kuendelea kuwa katika hali ya usafi.

Vijana waliojitokeza katika zoezi hilo wameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kufanya usafi na kutunza mazingira kwa njia zote.

Chanzo Michuzi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments