WAANDISHI WA HABARI SIMIYU WAMTUNUKU CHETI CHA HESHIMA MBUNGE NJALU

 

Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu (SMPC) kupitia mkutano wake Mkuu maalumu uliofanyika leo Desemba 30,2022 Mjini Bariadi, imemtunuku Cheti Cha heshima mbunge wa Jimbo la Itilima Mkoani humo Njalu Silanga (CCM) kutokana na mchango wake uliotukuka kwenye taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 mpaka sasa.


Kabla ya kumkabidhi Cheti hiyo cha heshima, Mwenyekiti wa Klabu hiyo Frank Kasamwa, amemtaja Mbunge huyo kama mdau mkubwa kwenye Klabu hiyo ndani ya Mkoa, kwani amekuwa msaada Mkubwa katika kuhakikisha Klabu na waandishi wa Habari wanafanya kazi katika mazingira mazuri.


Amesema kuwa Klabu pamoja na wanachama wake Kuna nyakati wamekuwa wakipitia kipindi kigumi, lakini mbunge huyo amekuwa pamoja nao wakati wote, huku akiwa mstari wa mbele katika kusaidia kutatua baadhi ya Changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.


" Kama Klabu Mheshimiwa Mbunge, tunakushukuru sana, ndiyo maana Leo tumeona tukutunuku Cheti hiki Cha heshima kwa kutambua mchango wako Mkubwa kwetu, umekuwa kiongozi na mwasiasa wa kuingwa, umekuwa kiongozi mwenye msaada mkubwa kwa Klabu yetu, lakini pia kuwa msaada mkubwa kwa wanachama ambao wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali" Amesema Kasamwa.


Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo, amewashukuru Viongozi, na wanachama wa SMPC kwa kutambua mchango wake, huku akihaidi kuendelea kuwa mtetezi wa waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu kila wakati.


Aidha Mbunge huyo amehaidi kuendelea kutatua Changamoto mbalimbali zilizopo kwenye Chama ikiwemo tatizo miradi ya kuendesha Klabu, huku akihaidi kuwa mlezi wa Klabu hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments