Recent-Post

Waomba msaada wa Serikali viboko kuvamia makazi

Uongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Bethany Child Care wilayani Busega mkoani Simiyu umeiomba Serikali kuingilia kati changamoto ya viboko wanaotoka ziwani kuvamia makazi yao.


 Changamoto ya viboko kuvamia makazi ya watoto kituoni hapo imebainishwa katika taarifa ya kituo hicho iliyosomwa na John Paul leo Desemba 24, 2022.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa viboko wamekuwa wakitoka ziwani na kuharibu mazao pamoja na kusogea karibu na makazi ya watoto nyakati za usiku, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto.Post a Comment

0 Comments