JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA SINGIDA IKOTAYALI KUENDELEZA KUTEKELEZA ILANI CCM MKOA WA SINGIDA.

            
           
             
  Pcha Ni Wakati Wa Kuhesabu Kura baada ya Uchaguzi Mdogo Uliofanyika katika baraza hilo
Omary Hamisi Akiongea na Viongozi Wenzake Wa Kamati Ya Utekelezaji Ya Jumuiya Ya Wazazi Mkoa Wa Singida ,Tayari Kwa Kuendelea Kutekeleza Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Wa Singida.
               
         
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM  Mkoa wa Singida, Bi.Bertha Nakomolwa akizungumza katika Kikao Cha Baraza la wazazi  na  Kamati ya utekekezaji Ya  Jumuiya Ya Wazazi Mkoa Wa Singida.
          
         
Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida, Bi.Bertha Nakomolwa  akipata picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Utekelezaji Wa Baraza la Wazazi Mkoa Wa Singida.

          
Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji wametakiwa kuendeleza mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinatendeka kupitia Ilani ya CCM ili wanachama na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na imani na Chama hicho.

Ameyasema hayo leo Januari 12,2023  Mwenyekiti wa  Jumuiya Ya Wazazi CCM   Mkoa wa Singida . Bi.Bertha Nakomolwa  Katika Balaza la wazazi lilofanyika offisi Za CCM Mkoa Wa Singida. 

Amesema kuna umuhimu wa viongozi wa chama hicho kuhakikisha kamati ya Siasa kutoa hamasa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha Chama hicho kinafanya vizuri katika chaguzi zijazo.

Aidha Bi.Bertha Nakomolwa  amewataka viongozi hao kushuka kwenye kata, wilaya na matawi kutoa elimu kuhusu masuala ya chama hasa Ilani ya Chama na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa Singida

Amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za uanachama ingawa wanachama wengi wanaingia kwenye chama hicho hivyo ameshalifikisha kwenye uongozi wa juu na linashughulikiwa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Bi Lucy Shee  amewasihi kamati ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kuhakikisha wanatumia michango kutekeleza miradi mbalimbali ili Juhudi za Jumuiya ya Wazazi zionekane na wanachama kuwa na imani na Chama hicho.

Katibu wa CCM Mkoa wa SingidaBi. Lucy Shee  Amewataka viongozi wa kamati ya Utekelezaji kuwa kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa  Singida  na kwa wananchi wa mkoa huo kwani ndani yenu wamo vijana, wanawake,hivyo wametakiwa kuhakikisha Chama kinakuwa imara.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments