Kamati ya kuangalia hali ya uchumi kwenye vyombo vya habari imeanza kazi rasmi ambayo itadumu kwa muda wa miezi mitatu.
Kamati ya kuchunguza hali ya uchumi ya vyombo vya habari iliundwa na Waziri mwenye thamana ya habari Nape Moses Nnauye ambayo kamati hiyo ilipewa hadidu za rajea.
Akizungumza wakati wa Uzindizi wa Kamati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla amesema ni mategeo ya serikali kupata matokeo ya kamati hiyo kutokana na hadidu za rejea walizopewa.
Amesema kamati itafanya kazi ambayo serikali watapokea na kufanyia kazi katika kuboresha masuala ya uchumi kwenye sekta uwekezaji wa habari nchini.
Aidha amesema kuwa wajumbe wa sekta ya habari wamebaba jambo kubwa katika nchi hivyo wanatakiwa kuliendea katika ujenzi wa taifa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali Grayson Msigwa amesema kuwa wajumbe waliopo kwenye kamati ni wabobevu hivyo ni imani watafanya kazi kwa weledi wa kuijenga tasnia ya habari.
Amesema miaka hivi karibuni sekta ya habari imekuwa katika mdororo wa uchumi hivyo serikali ya awamu ya Sita ya Dk.Samia Hassan Suluhu ikaona kuna jambo la kufanya katika sekta ya habari nchini.
Mwenyekiti wa Kamati Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa wamepewa jukumu watalifanyia kazi na wajumbe na kupeleka serikalini kwa ajili ya utekelezaji.
Kamati yetu pamoja na waandishi wawe na imani kwenye hili kwani kazi itafanyika na kupeleka kunako husika kwa ajili ya utekelezaji
Wajumbe kamati hiyo Mwenyekiti Tido Mhando (Azam Media), Joyce Mhavile Mkurugenzi Mtendaji ITV, Keneth Simbaya Mkurugenzi wa Jumuiya ya Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) Rose Reuben Mkurugenzi wa TAMWA, Richard Mwaikenda Mwaindishi Mkongwe , Sebastian Maganga Clouds Media.
Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla akifungua kikao cha Kwanza cha Kamati ya Kuangalia Uchumi wa vyombo vya habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuangalia hali ya uchumi Tido Mhando akizungumza namana itavyofanya kazi kwa muda uliopangwa jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mohamed Khamis Abdulla akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya kuangalia hali ya uchumi katika vyombo vya habari mara baada ya kikao cha kwanza kufunguliwa jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mohamed Khamis Abdulla akiwa katika picha ya kamati ya kuangalia hali ya uchumi katika vyombo vya habari pamoja na Sekretarieti mara baada ya kikao cha kwanza kufunguliwa jijini Dar es Salaam.
0 Comments