Lissu, Lema na Wenje kurejea nchini mwezi huu

Wakati Chadema ikitarajia kuzindua mikutano ya hadhara Januari 21, mwaka huu, viongozi wake walioko nje ya nchi, Tundu Lissu, Godbless Lema na Ezekia Wenje wanatarajiwa kuwa miongoni mwa washiriki katika mikutano hiyo, Mwananchi limedokezwa.

Mikutano ya hadhara ya chama hicho inatarajiwa kuanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, mbele ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, kutangaza Januari 3 mwaka huu kuondoa zuio lililokuwepo.

Zuio hilo liliwekwa mwaka 2016 na Rais wa wakati huo, John Magufuli akitaka mikutano hiyo ihusishe wabunge na madiwani pekee waliochaguliwa, huku wengine wakitakiwa kufanya mikutano ya ndani ambayo nayo wakati mwingine ilikuwa inazuiwa


Mikutano ya hadhara ya chama hicho inatarajiwa kuanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, mbele ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, kutangaza Januari 3 mwaka huu kuondoa zuio lililokuwepo.

Zuio hilo liliwekwa mwaka 2016 na Rais wa wakati huo, John Magufuli akitaka mikutano hiyo ihusishe wabunge na madiwani pekee waliochaguliwa, huku wengine wakitakiwa kufanya mikutano ya ndani ambayo nayo wakati mwingine ilikuwa inazuiwa


Katika kusisitiza hilo, mjumbe huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, “lakini unaweza kuwacheki sasa Lissu na Lema wenyewe watakwambia maandalizi yao yamefikia wapi lakini kwenye uzinduzi wa mikutano watakuwepo.”

Ingawa Chadema haijaweka wazi uzinduzi huo utafanyikia wapi, gazeti hili lina taarifa kwamba utafanyika katika Kanda ya Mashariki yenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Mikutano itaanza Dar es Salaam kisha kwenda kanda zingine. Na Chopa ‘helkopta’ itatumika kwa ujumbe wa mwenyekiti Mbowe ambaye atafanya uzinduzi kanda zingine tisa na baada ya hapo mikutano itakuwa kila mahali,” kilidokeza chanzo chetu.

Alipoulizwa kwa simu kama atakuwepo katika uzinduzi wa mikutano hiyo, Lissu alijibu kwa ufupi, “nitarejea nyumbani muda si mrefu kaka, tutatoa taarifa rasmi muda si mrefu.”

Wakati Lisu akisema hivyo, Wanje kwa upande wake alipoulizwa alikiri suala hilo kuzungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu na kuwa wamekubaliana kurejea nchini.

Alisema Lissu ndiye atakayetangulia na wengine watafuatia.

“Lissu atatangulia kisha mimi nitaingia Februari 5 na tayari tiketi nimeshakata. Kweli tungeweza kuja siku ya uzinduzi wa mikutano, lakini unajua tena mambo ya ratiba binafsi,” alieleza Wenje anayeishi Marekani.

Wenje alisema kwa kuwa mikutano imesharuhusiwa, kurejea kwao kutaongeza nguvu katika maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025, kupitia majukwaa ya siasa.

Jitihada za kumpata Lema hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopokewa na ujumbe uliotumwa kwake haukujibiwa.


Kauli ya Chadema

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema kina Lissu waliondoka wakiwa na sababu za msingi, hivyo hata kurejea nchini lazima wajiridhishe kama mazingira ni salama.


“Kama chama tungetamani wote tuwepo tuijenge Chadema ili tujiandae na 2025, haya ndiyo matamanio ya chama na ushauri ni kwamba kama wanaweza kurejea warejee.

“Hatuoni tatizo lolote kwa sasa, lakini haya mambo kwa kuwa mwisho wa siku yanamkuta mtu binafsi, lazima ajiridhishe kwa nafsi yake. Lakini Chadema hatuoni tatizo lolote bahati nzuri Lissu siku nyingi alitangaza kurudi baada ya Serikali kusema hali ni salama,” alisema Mwalimu aliyekuwa mgombea mwenza wa Lissu katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments