Majaliwa avutiwa ushirikiano CCM, Chadema na ACT-Wazalendo

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani ameonesha nia ya kuvitaka vyama vya siasa kuwa kitu kimoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Rais Samia aliyeingia madarakani Machi 19, 2021 akirithi mikoba ya hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 wakati akipatiwa matibabu Dar es Salaam.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ikulu Dar es Salaam, Januari 3, 2023 katika kikao cha Rais Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM na viongozi wa vyama vya siasa 19 vyenye usajili wa kudumu akisema hivi sasa kumeshuhudiwa mahusiano mazuri ya viongozi wa vya


“Hata leo tumeshuhudia katika chombo kimoja cha habari ikionyesha viongozi wa vyama siasa kule mkoani Iringa, akiwemo Richard Kasesela (mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM) mchungaji Peter Msigwa (Mjumbe wa kamati kuu Chadema) na Peter Ndolezi (mjumbe wa baraza Kuu la ACT), wakisimama kuunga mkono jitihada za Rais kuhusu uhifadhi wa mazingira.

“Kwa kitendo kile au tukio lile sasa tunaanza kushuhudia tukisimama pamoja kwa masilahi ya Taifa letu, sisi tupo tayari kuyafanyia kazi maelekezo utakayoyatoa,” amesema Majaliwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments