MKUTANO MKUU WA SIREFA 2022 WAFUFUA MABADILIKO MAKUBWA YA SOKA MKOANI SI...

Vyama vya Mpira wa Miguu vya Wilaya Mkoani Singida vimetakiwa kusimamia Sera ya michezo ya kuendesha mashindano mbalimbali katika maeneo yao ili kukuza vipaji kwa vijana kuanzia ngazi ya Wilaya huku msisitizo ukiwa katika soka la wananwake.

Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida Amani Mwaipaja Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Singida SIREFA ambao umefanyika  Jana  Desemba 31 2022 katika Chuo cha Maendeo ya Wananchi FDC uanzishwaji na usimamizi wa michezo  katika maeneo husika huku Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Mkoani Hapa  Yagi Kiaratu akitilia mkazo Suala hilo.

                     

“Kwenye vyama vya wilaya tuongeze nguvu katika kufanya mashindano, tunaweza tukawa tunaandaa mshindano kulingana na Geografia zetu mfano watu wa Iramba kuna center kama Kiomboi, Shelui na Ulemo tunaweza tumia center hizo tukapata timu zinazoweza kushiriki ligi ya wilaya hadi ya Mkoa”, 
Alisema Mwaipaja.

Alisema Serikali kupitia kwa Waziri imeendelea kusisitiza mashindano mbalimbali kufanyika ngazi ya chini lengo likiwa ni kuibua vipaji kuanzia umri mdogo ambao watoto wanapokuwa shule wakijengewa misingi bora ya kushiriki michezo mbalimbali hasa Soka.

Sanjari na Hayo Afisa huyo wa michezo Mwaipaja alisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyama vya soka mkoani hapa ili kuleta mabadiliko ya soka.


Mwenyekiti wa chama cha Soka la Wanawake Mkoani Singida Yagi Kiaratu alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Singida Umekuwa ukitolewa mfano katika uendeshaji ligi ya wananwake mkoani hapa hivyo alivitaka vyama vya soka ngazi ya wilaya kuekeza nguvu Zaidi ili kuibua vipaji kupitia soka la wanawake.

Mgeni Rasmi katika Mkutano huo wa SIREFA Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TFF kanda ya Kati Mohemed Aden ameahidi Kuwezesha Mafunzo ya Makocha mkoani Singida Ngazi ya Awali na kutoa wito walimu wa shule za msingi kujitokeza kushiriki kozi hiyo

Aden Alisema kuwa Makocha wengi wanaofundisha watoto bado wa elimu iliyopitwa na wakati hivyo akahidi kuleta kozi hiyo kuhu akitoa kipaumbele kwa walimu wa shule za msingi kusoma kozi hiyo kwani wao ndio wanaoanza kuajenga watoto wakiwa wadogo shuleni.

“Nimeongea na Mwenyekiti amsema makocha wengi elimu ambayo kwa sasa kama imepitwa na wakati hivyo nitaangalia uhitaji wa walimu na nitaleta kozi ya Grass root (Kozi ya ukocha ya Awali) kwa gharama zangu mimi mwenyewe”, Alisema Aden

“Na nitoe wito tu kwa walimu wa shule za msingi wajitokeze kwa wingi kusoma kozi hiyo pindi itakapotangazwa na SIREFA ili wapate kuwasaidi watoto kwa sababu watoto wamekuwa wakiumia na ndoto zao za kucheza zinaishia njiani”, Aliongeza Mjumbe huyo wa kamati Tendaji ya Tff

Kuhusu Suala ya idadi ya Mashindano likatiliwa mkazo na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Singida SIREFA Hamis Kitila ambaye alivita vyama vya Soka vya Wilaya Kuongeza idadi ya hasa kuanzia mwaka mpya wa 2023 na kusema kuwa mashindano kuwa na timu chache katika eneo husika haitakubalika kulingana na taratibu zao.

Mwenyekiti Akipokea Zawadi  Jezi Na Mipira Kutoka kwa Mgeni Rasmi

Hamis Alisema SIREFA kwa kushirikiana na Ofisi ya Ofisa Michezo wataunda kamati za Wilaya zitazokuwa zinafuatilia kutambua mashindano yote yanayofanyika yasiyorasmi na yaliyo rasmi ili kuleta mabadiliko katika soka.

“ Hili Suala ya timu Sita katika Mashindano halitakubalika, sisi singida mashindano kuwa yana timu 24 sasa  sasa timu chache halitavumilika, na tunampango wa  kuwa na barua kwa kushirikiana na afisa michezo kuyatambua mashindano yote yaliyorasmi na yasiorasmi hivyo tutaunda kamati zitakazo simamia hilo”, Alisema Kitila.

Akizungumza kwa Niaba ya wajumbe wa mkutano huyo wa SIREFA Mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Manyoni Rajabu Mlosha ameiomba Sekretarieti ya SIREFA kupunguza kwa ada ya kiingilio cha Ligi ya Mkoa ili kuongeza idadi ya timu shiriki kwa kiasi cha Shilingi 300000/ ni kikubwa  ulinganisha na mapato ya vilabu vinavyotaka kushiriki ligi ya Mkoa.

Katika hatua nyingine Mkutano huo wa SIREFA  ulitoa taarifa ya mikakati ya kujenge Uwanja wa Kisasa wa kufanyia Mazoezi ambayo eneo lenye ukubwa wa Ekari 4 limepatika Mtaa wa Manga  na tayari  mchakato wa kujenga uwanja huyo zimeanza jambo ambalo wananchama wa SIREFA limewafurahisha.

Mkutano Mkuu wa SIREFA umefanyika jana Desemba 31 2022 katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi FDC Ikishirikisha wanachama kama Chama cha Soka Wilaya ya Singida Mjini SIDIFA, Chama cha Soka Wilaya ya Manyoni (MADIFA), Chama cha soka Wilaya ya Iramba (IRADIFA) , chama cha waamuzi (FRAT) chama cha Makocha TAFCA, chama cha soka la wanawake Mkoani Singida TWFA, Sekretarieti na Kamati Tendaji ya SIREFA.










TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments