MUDATHIR ATUA YANGA SC

KIUNGO mahiri kutoka visiwani Zanzibar, Mudathir Yahya Abbas rasmi amekamilisha usajili katika Klabu ya Yanga baada ya kuondoka Azam FC, hata hivyo haijawekwa wazi Mudathir amesaini mkataba wa muda gani.

Mudathir amesaini mkataba huo mchana wa leo (Januari 3, 2023) katika Ofisi za Klabu hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam huku tukio hilo likishuhudiwa na Rais wa Klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Andre Mtine.

Kiungo Mudathir Yahya tayari amepanda Boti kuelekea visiwani Zanzibar kujiunga na timu hiyo ambayo ipo huko kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2023 ambapo Yanga SC wataanza kucheza dhidi ya KMKM siku ya Januari 4, 2023.

Mudathir Yahya ni Kiungo wa Kizanzibar katika ardhi ya Tanzania Bara amewahi kucheza Klabu za Singida United ambayo sasa inafahamika kwa jina la Singida Big Stars na Azam FC, pia mara kadhaa ameitwa kwenye Kikosi cha timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars).


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments