MWENYEKITI CCM MKOA SINGIDA AFUNGUKA RAIS SAMIA KURUHUSU MIKUTANO YA HADHARA


Mwenyekiti Wa CCM M koa Wa Singida Martha Mlata
                    
Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa  Singida Marta Mosses  Mlata
amesema hatua aliyochukua Dr.  Rais Samia Suluhu Hassan ya kutengua
katazo la mikutano ya hadhara inathibitisha ukomavu alionao , weledi,
uthubutu na nia nzuri ambayo kwa Watanzania.

Martha   Mlata ameyasema hayo leo Januari 5,2023  Mkaoni Singida 
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyochukuwa
na Rais Dk.Samia kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa
nchini.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa vyama vyote vya
siasa ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa jitihada ambazo amekuwa
akizifanya tangu aingie madarakani za kuhakikisha mazingira ya
ufanyaji siasa yanaboreshwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha hali ya
demokrasia , uhuru wa vyombo vya habari , uhusiano na vyama vya siasa
pamoja na uhuru wa kujieleza.

“Ni ukweli kuwa jitihada , nia na uthubutu wake situ umekuwa nguzo
muhimu ya kuchochea kasi ya mariadhiano ya kisiasa nchini bali
zimechangia pakubwa kuondoa mkwamo wa kisiasa ulioshuhudiwa kwa miaka
sita sasa.Hatua iliyochukuliwa na Rais Samia kuruhusu mikutano ya
hadhara kwa vyama vya siasa inathibitisha ukomavu alionao,”amesem Martha

Amesema CCM Mkoa wa Singida  kinaamini kuruhusiwa kwa mikutano ya
hadhara kutaimarisha nguvu za kisiasa za Chama hicho, kutapanua wigo
kwa wanachama wengi zaidi kutoa mawazo chanya kuhusu masuala
yanayohusu Taifa lao na kufungua fursa kwa viongozi wa ngazi wa Chama
wa ngazi zote kunadi na kutangaza hadharani mazuri yote
yanayotekelezwa na Serikali.

Aidha amewaomba watanzania wote kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Samia
, kumuombea afya kwa Mungu , busara na maono zaidi ili aendelee
kulifanyia Taifa mambo makubwa zaidi.

“Ni dhahiri kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake amefanya
mambo makubwa kwenye sekta ya miundombinu , afya , elimu , ulinzi na
usalama, demokrasia , uhusiano wa kimataifa pamoja na uhuru wa vyombo
vya habari,”amesema Martha Mlata

Ametumia nafasi hiyo kueleza wana CCM Mkoa wa Singida  wanamuahidi Rais
Samia na Watanzania kwa ujumla kuwa watafanyasiasa za kistaarabu
zisizo na lugha za maudhi , vurugu , maandamano yasiyo na lazima ili
kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa maslahi mapana ya  Jamiin Na Taifa Kwa Ujumla.
                          
Ccm Mkoa Wa Singida Tunakukaribisha Kwa Mikono Miwili Kwa Uamuzi Huo ,Tupo Tayari Kwa Hoja Za Viama Vingine Katika Majukwa Kwa Kuzingatia Utekelezaji  Mzuri Wa Ilani Unaoendelea Mkaoni Singida, Asema Mwenyekiti Wa Ccm Mkoa Wa Singida Martha Mosses Mlata.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments