MWIGULU NCHEMBA: KODI NA TOZO NI SEHEMU YA KUKUZA UCHUMI WA NCHI

 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akifungua Kongamano la Kodi la Kitaifa katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo la kwanza kuwahí kufanyika nchini limelenga kukusanya maoni mbalimbali kuhusu mfumo wa kodi, ulipaji wa kodi wa hiari na Maboresho ya sera kwa maendeleo ya watu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Lawrence Mafuru akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano  la kwanza kuwahí kufanyika nchini ambalo limelenga kukusanya maoni mbalimbali kuhusu mfumo wa kodi, ulipaji wa kodi wa hiari na Maboresho ya sera kwa maendeleo ya watu.

Mbunge wa jimbola Vunjomkoani Kilimanjaro Dkt. Charles Kimei akitoa mchango wake katika Kongamano la kwanza kuwahí kufanyika nchini ambalo limelenga kukusanya maoni mbalimbali kuhusu mfumo wa kodi, ulipaji wa kodi wa hiari na Maboresho ya sera kwa maendeleo ya watu.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akifafanua hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wadau katika Kongamano la Kodi la Kitaifa katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam kulia ni Saada Mkuya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.

Baadhi ya wadau mbalimbali wakisikiliza kwa umakini mada mbalimbali wakati wa Kongamano la kodi la kitaifa la kwanza kuwahí kufanyika nchini lenye lengo la kukusanya maoni mbalimbali kuhusu mfumo wa kodi, ulipaji wa kodi wa hiari na Maboresho ya sera kwa maendeleo ya watu.

Picha ya pamoja.

Kodi Pamoja na tozo mbalimbali ni sehemu ya kukuzia uchumi wa Nchi endapo wananchi  wataelimishwa vizuri  umuhimu wa kulipa kodi na ni muhimu Tunapotafakari Hapa tutafakari na kuona umuhimu wake.

Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo Leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye Kongamano la Kodi la kitaifa lenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa wadau katika ukusanyaji wa maoni Kwa ajili ya maandalizi ya Bajeti Kwa Mwaka 2023/2024.

Dkt. Mwigulu amesema kuwa Kwa mujibu wa historia mambo mengi yalikuwa yanawezwa kufanywa na serikali jambo ambalo watu wakawa na imani ya kuwa serikali inawaajiri wanafunzi kila wanapomaliza vyuo.

Aidha meongeza kuwa mtazamo wa Mhe Rais pindi anapotokea Mtu anaanzisha shughuli za uzalishaji ni vyema watumishi wa serikali wakaonyesha ushirikiano kwa wadau hao ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto walizonazo ili kuzikwamua waweze kujikwamua kwa kupitia Masuala ya kodi na tozo za serikali.

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Laurence Mafuru amesema wataendelea kushirikiana na sekta binafsi kwani ndio mwajiri na mzalishaji mkubwa katika nchi.

Amesema serikali imekuwa ikiwashirikisha wadau wa sekta binafsi katika mchakato wa kuanza kutengeneza sera za Kodi Ili kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa Nchi.

“Tunaweza kupanga matokeo ya kodi na mawazo yatakayopatikana  ndio yatakayotumiwa na Timu yetu ya Wataalamu ambayo inaandaa sera za kodi kwa mwaka ujao wa Fedha,”amesema  Lawrence Mafuru.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments