Ikiwa imebaki siku moja kufunguliwa kwa shule zote nchini Tanzania, Jeshi la Polisi nchini humo limewataka wazazi na walezi kuhakikisha, wanaweka utaratibu mzuri wa watoto hao kwenda na kurejea nyumbani.
Pia, Jeshi hilo limewataka madereva na makondakta wa daladala waepuke vitendo vinavyoweza kuwaumiza watoto kimwili au kisaikolojia na kuwanyima haki zao za kimsingi.
Shule za msingi na sekondari, zitafunguliwa Jumatatu, Januari 9, 2023.

Pia aliwataka kujiepusha na matendo ya uzembe yanayoweza kuhatarisha usalama wa watoto wanaokwenda na kurudi shule.
’Tunatoa wito kwa wananchi wote tushirikiane kuwalinda watoto wetu, tukumbuke ukimjali na kumlinda mtoto wa mwenzio na wa kwako wengine watamjali na kumlinda,” amesema Misime.
0 Comments