Taarifa iliyotolewa jana, Januari 5, 2022, Kafulila ameteuliwa kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), ikiwa ni miezi 6 tangu Julai 28, 2022 alipoachwa katika teuzi za Wakuu wa Mikoa.
Mbali wadhifa wa Mkuu wa Mkoa, Kafulila amewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe na amewahi kuwania ubunge lakini alishindwa katika kura za maoni CCM.
Wengine katika uteuzi huo ni Dk Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Justine Mwandu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Yumo, Profesa Verdiana Masanja aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), Griffin Mwakapeje kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania na Fatma Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy nchini Geneva.
0 Comments