Recent-Post

TFF: FEITOTO NI MCHEZAJI WA YANGA SC

 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum (Feitoto) ni bado ni Mchezaji wa Yanga SC kwa mujibu wa mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi kamili wa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu, Januari 9, 2023.

Aidha taarifa hiyo imeeleza imeelezwa kuwa Yanga SC iliwasilisha taarifa hiyo mbele ya Kamati hiyo ikidai kuwa Feisal Salum alivunja mkataba baina yao bila kuwashirikisha.

Kamati hiyo ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikikiza shauri hilo hapo jana (Januari 6, 2023) pande zote mbili Feisal na Yanga SC waliwakilishwa na Wanasheria wao. 


Post a Comment

0 Comments