VIONGOZI VYAMA VYA SIASA WAWASILI IKULU KUKUTANA NA RAIS DK.SAMIA SULUHU HASSAN

 VIONGOZI mbalimbali wa vyama vya siasa tayari wamewasili katika Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.


Miongoni mwa viongozi ambao wamehudhuria mkutano huo ni pamoja na wenyeviti , makamu wenyeviti na makatibu wakuu na katika mkutano huo kunatarajiwa kujadiliwa masuala mbalimbali ya kisiasa nchini ikiwa ni muelekeo mpya wa Rais Samia katika kuboresha siasa za Tanzania.

Kwenye mkutano huo pia viongozi kadhaa akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC Hamad Rashid Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Juma Duni Haji,Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Kabla ya mkutano wa leo kati ya Rais Dk.Samia na viongozi wa vyama vya siasa, tayari kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi wa vyama hivyo na kujadiliana masuala mbalimbali huku akiunda tume maalumu ambayo inaratibu masuala ya kisiasa nchini na miongoni mwa mambo yanayopewa nafasi kubwa kujadiliwa ni kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.

Kwa muda mrefu kumekuwepo na zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kukutana na wanachama wao pamoja na wananchi, hivyo kwenye mkutano wa leo vyama vya siasa wanatamani kusikia kauli ya Rais Samia kwenye eneo la mikutano ya hadhara kama itaruhusiwa au laa.

Ajenda nyingine ambayo viongozi wa vyama vya siasa wanatamani kuisikia ikitolewa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan ni mchakato wa kupata Katiba mpya ambao kwa muda mrefu umekuwa ukipigiwa kelele na wanasiasa sambamba na Tume huru ya Uchaguzi.

Hivyo endelea kufuatilia Michuzi TV na Michuzi Blog ambayo itakupa kila kinachoendelea ndani ya mkutano huo ambao unatarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa.Tuko Ukumbi wa mikutano Ikulu kwa ajili ya kukujuza kila kinachoendelea.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA  Ndugu Freeman Mbowe mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 3,2023 kwa ajili ya kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan,Pichani kulia ni Mwenyekiti wa chama cha CUF Profesa Ibrahimu Lipumba. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments