WAKULIMA KILOMBERO WATOA MALALAMIKO YAO KWA KATIBU MKUU CCM KUHUSU UTAMU WA MUWA KWENYE MALIPO

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amepokea malalamiko ya wananchi ambao wanajihusisha na wakulima wa miwa Kilombero mkoani Morogoro ambao wamedai kukosa imani na Kiwanda cha sukari Kilombero kwa jinsi wanavyopima kiwango cha utamu wa miwa wauzayo kiwandani hapo.


Kwa mujibu wa wakulima hao ni kwamba malipo ya fedha yamekuwa yakitolewa kwa utamu wa miwa ,hivyo wamekuwa wakilipwa malipo madomo ambayo yamekuwa yakisababisha malalamiko hayo.

Wametoa malalamiko hayo leo kwa Katibu Mkuu Chongolo ambaye yupo mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tisa akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC )ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Sophia Mjema ambapo pamoja na kukugua uhai wa Chama wameendelea kusikiliza changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kilombero, Mbunge wa Kilombero, Abubakar Assenga, amesema changamoto kubwa ni mgogoro baina ya wakulima wa miwa na kiwanda cha Kilombero.

Ameongeza kwamba mgogoro mkubwa umekuwepo kwenye kiwango cha utamu wa muwa (Sucrose), malipo ya mkulima anayekwenda kuuza miwa yake kiwandani hapo yanategemea utamu wa muwa, sasa wakati kupima hakuna mkulima anayepewa fursa ya kujua bali anaambiwa utamu wa muwa ni mdogo na malipo yanakuwa madogo."Mgogoro huo ni wa muda mrefu na viongozi wengi wamepita, lakini tatizo liko palepale."

Akizungumza kuhusu malalamiko hayo, Chongolo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kutengeneza utaratibu wa kukaa na Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Biashara(Amcos), viteue wakulima mmoja mmoja wafundishwe jinsi ya kufahamu upimaji wa kiwango cha utamu wa sukari, ili kuondoa manung'uniko yao.

Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwenye Ziara hiyo ameambatana na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu kwa ajili ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho pamoja na kuzungumza na Makundi mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na baadhi ya wakulima wa Shamba la Miwa la Tawi la CCM Sanje kata ya Sanje ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Chongolo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu), pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali kutoka mkoani humo na Wilaya ya Kilombero
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wakulima wa Shamba la Miwa la Tawi la CCM Sanje kata ya Sanje ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro. 

 Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu), akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wakulima wa Shamba la Miwa la Tawi la CCM Sanje kata ya Sanje ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro. 

Mbunge wa jimbo la Kilombero, Abubakar Assenga akiwasilisha  changamoto kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo kuhu mgogoro baina ya wakulima wa miwa na kiwanda cha Kilombero.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments