WAKUU WA WILAYA WAPYA WATAKIWA KUHESHIMU VIAPO VYAO.

 Katibu  Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Jasmini Awadhi amewataka wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa kuheshimu na kuviishi viapo vyao walivyoviapa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ktk utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. 


Bibi Awadhi alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa kiapo cha  Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa wilaya ya Chemba  Gelard Lomward Mongela  katika hafla fupi iliyofanyika  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma tarehe 30 January 2023.

Alisema"hakikisheni mnajitoa kutumikia viapo mlivyotoa mbele yetu na kuviweka katika kumbu kumbu zenu za kila siku ili viwasidie kuyakunbuka yale yote yaliyoelezwa katika viapo hivyo mnapotekeleza majukumu yenu ya kila siku".

Katika hatua nyingine  Bibi Awadhi alimpongeza Mkuu wa wilaua ya Chemba  kwa kuteuliwa kwake na alisema kuwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekupa heshima ya kubwa ya kuiongoza wilaya ya Chemba.

Katibu huyo Msaidizi aliwapongeza wakuu wengine wapya wa wilaya za Bahi Mhe Godwini Gondwe na Mpwapwa Mh Sophia Kizigo waliohamishiwa mkoani Dodoma katika mabadiriko ya vituo vya wakuu wa wilaya yaliyofanyika hivi karibuni.

Hafla ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Chemba na kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya ilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyemule ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Dodoma, Viongozi  wa dini, Viongozi wa vyama vya siasa, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na Menejimenti ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Katibu  Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Bibi Jasmini Awadhi akizungumza wakati hafla ya uapisho kwa wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dodoma.Katibu  Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Bibi Jasmini Awadhi akishuhudia kiapo cha mmoja wa wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dodoma Katika hafla ya kiapo  hicho kilichofanyika Ofisi ya Mkuu  Mkoa wa Dodoma. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments