Watu 9 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kukanyagana kwenye Msongamano ulitokea Freedom City Mall usiku wa kuamkia Mwaka Mpya 2023.
Akithibitisha tukio hilo Naibu msemaji wa polisi wa Metropolitan ya Kampala, Luke Owoyesigyire amesema kuwa waathiriwa walikandamizwa huku mamia ya watu wakijaribu kurejea ukumbini baada ya kutazama onyesho la fataki lililoanzisha mwaka mpya.
"Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati MC wa hafla hiyo aliwahimiza waliohudhuria kutoka nje na kutazama maonyesho ya fataki. Baada ya onyesho kumalizika, mkanyagano ulitokea, na kusababisha vifo vya papo hapo vya watu watano na wengine kadhaa kujeruhiwa,” Owoyesigyire alisema.
Amesema sehemu ya duka hilo imefungwa ili kuruhusu uchunguzi wa tukio la jana usiku lililowaua tisa.
"Ni sehemu tu ambayo tukio la jana usiku limefungwa ili kuruhusu uchunguzi. Eneo hilohilo lilikuwa na tukio lingine lililopangwa kufanyika leo lakini haliwezi kutokea kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea kwenye eneo la uhalifu,” Owoyesigyire aliambia Nile Post.
Hata hivyo alibainisha kuwa sehemu nyingine za maduka hayo ikiwa ni pamoja na maduka makubwa na vifaa vingine bado viko wazi na biashara bado inaendelea.
Ziara katika jumba hilo la maduka Jumapili alasiri inaonyesha kuwa baadhi ya washiriki wa sherehe hizo wakiwemo watoto waliokuwa wamefika kwenye bwawa la kuogelea wamerudishiwa pesa zao kwani mahali hapo bado ni eneo la uhalifu.
0 Comments