Ajali yaua 12, majeruhi 63 Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani hapa, Remidius Mwema amesema watu 12 wamefariki dunia huku majeruhi wakiwa 63 kwenye ajali ya basi na lori wilayani Kongwa.

Akizungumzia ajali hiyo leo Alhamisi Februari 9, 2023 Mwema amesema ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Sirwa, Kata ya Pandambili wilayani Kongwa, imesababisha vifo 12, wanaume wanane na wanawake wanne.

Mwema amesema majeruhi wa ajali hiyo ni 63, wanaume 40 wanawake 23. Tayari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amefika eneo la tukio.

Ajali hiyo imehusisha basi la Frester lililokuwa likitokea Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam baada ya kugongana na lori uso kwa uso katika Kijiji cha Sirwa usiku wa kuamkia leo.


Amesema majeruhi 36 wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na wanne wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kuonekana wana matatizo makubwa.
Amesema majeruhi 27 walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kibaigwa ambapo kati ya hao 16 walihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu zaidi.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments