Baraza La Madiwani Wilayani Mkinga Lapitisha Bajeti Ya 2023/2024

 Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya mkinga lapitisha Kwa kauli moja makisio ya mpango na bajeti ya halmashauri Kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya shilingi 26,998,507,369 kwa utekelezwaji wa miradi ya maendeleo,ruzuru ya mishahara na matumizi wa kawaida.

Makisio hayo yalipitishwa katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya mkinga uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Akiwasilisha rasimu ya makisio ya mipango na bajeti ya halmashauri hiyo kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 mkurugenzi wa halmashauri wilaya ya mkinga Zahra msangi alieleza kuwa ni jumla ya shilingi 26,998,507,369 ambapo kati ya fedha hizo tsh 2,601,959,485 ni mapato ya ndani, shilingi 14,902,856,000, shilingi 869,919,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 8,623,772,884 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande Wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya mkinga Abdallah sengano alimpongeza Rais Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule na vyumba vya madarasa katika Shule za msingi ambapo mpaka sasa serikali inaendelea kutoa fedha.

Katika hatua nyingine kaimu katibu tawala wilaya ya mkinga Erick Farahami alieleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuona Mabadiliko mpaka 2025 ikiwa imeweka mikakati madhubuti ya kuleta maendeleo ya nchi.

"Ni kuwa Rais wetu samia suluhu Hassan anafanya kazi kwa juhudi na uzalendo kwenye Taifa letu lakini ni kuwa anatoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara,ujenzi wa madarasa,nyumba za wakurugenzi ikiwemo katika halmashauri yetu ya wilaya ya mkinga hivyo niwaombe madiwani wote kumisamia shuhuri za kiserikali ikiwemo ukusanyaji wa mapato Ili kumsaidia Rais Samia katika kufikia lengo husika". Alisema Eric Farahami

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya mkinga wakiwa katika mkutano wa Makisio ya bajeti ya 2023/2024 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mkinga Zahra msangi kulia akiwa na kaimu katibu tawala wilaya ya mkinga (kushoto)akitoa taarifa kuhusi makisio ya bajeti ya Mwaka 2023/2024 mbele ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya mkinga.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments