Basi lapata ajali Butiama, 20 wakimbizwa hospitali

Watu 20 wamelazwa katika Hospitali ya teule ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi la Africa Raha linalofanya safari zake kati ya Musoma na Mwanza.

Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Februari 12, 2023 saa 9 mchana katika kijiji cha Mwibagi wilayani Butiama katika barabara ya Mwanza Musoma.

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema kuwa majeruhi hao 20 wamekimbizwa katika hospitali hiyo na wanaendelea na matibabu.


"Tumepokea majeruhi 20 na watatu kati yao hali zao sio nzuri sana madaktari wanajitahidi kufanya kila wawezalo ili kuokoa maisha yao." amesema Dk Naano

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana kwa maelezo kuwa ajali hiyo imetokea wilaya ya Butiama.

"Wasiliana na watu wa Butiama sisi hapa tumepokea majeruhi tu taarifa za ajali bado hatuna, kwa sasa naweza kuongelea idadi ya watu waliolazwa hapa hospitalini." ameiambia Mwananchi  kwa njia ya simu.


Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments