BONANZA LA MICHEZO KUANZA RASMI FEBRUARI 25 - MSTAHIKI MEYA

Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow akiongea na waandishi wa habari.
Ofisa Tawala wa jiji la Tanga Mwanaidi Nondo.HALMASHAURI ya jiji la Tanga Ina mpango wa kuwakutanisha watumishi na watendaji wake katika michezo mbalimbali ili kujenga na kudumisha amani na pendo, pamoja na kujikinga na magonjwa ambayo yanaepukika.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow amesema wameandaa bonanza litakalo washirikisha watumishi, watendaji wakiwemo waheshimiwa madiwani wa kata zote jijini humo.


"Kama halmashauri tumeamua kuanzisha bonanza la michezo mbalimbali, lengo likiwa ni kuamsha ari ya watu wa Tanga wawze kuweka michezo kama kipaumbele chao katika shuhuli na maisha yao ya kila siku" amesema Shiloow.


"Kwahiyo siku ya jumamosi februari 25 tumeandaa bonanza litakaloshirikisha michezo mbalimbali kwa watumishi na watendaji wote ambalo litafanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Popatlal kuanzia majira ya saa 12 asubuhi" amefafanua.


Aidha Shiloow amebainisha kwamba mbali na kujenga amani kwa watumishi wa halmashauri hiyo lakini pia michezo inalinda afya na kuepusha magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa kama vile, kisukari, moyo, kisukari na mengineyo, hivyo kusisitiza watumishi hao kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza kwa manufaa ya afya zao.


Kwa upande wake Ofisa Tawala wa jiji la Tanga Mwanaidi Nondo amesema watumishi na watendaji wengine hawapati nafasi ya kujuana na kuzoeana kwa ukaribu wanapokuwa katika majukumu yao ya kila siku lakini watakapokuwa wakishiriki michezo kama hiyo watapata kuwa na ukaribu utakaowafanya kujenga umoja, Upendo mshikamano na amani.


"Katika kuelekea kwenye maandalizi ya bonanza hili kutakuwa na zawadi kwa washindi wataoshiriki, lakini pia kwa sababu tunasema michezo ni afya, tumeandaa mabanda ya kupimia afya katika viwanja hivyo ili watu wapime afya zao lakini kutakuwa na uchangiaji wa damu salama" amesema.


"Na kwakuwa matangazo ya bonanza hili yameshawafikia watumishi wengi mpaka kwenye mitaa, napenda kutoa msisitizo kwa watumishi bila kujisahau, wake kwa wingi siku ya jumamosi waungane na kushirikiana katika kudumisha bonanza hilo ambalo litakuwa ni endelevu, hivyo kila februari 25 ya kila mwaka litafanyika hapa" ameongeza.


Naye Ofisa Michezo wa jiji hilo Michael Njaule amesema bonanza hilo litawakutanisha wtumishi wa halmashauri, walimu wa shule za msingi na sekondari, wahuduku wa afya, watendaji wa mitaa pamoja na wakuu wa idara.


"Tumesha vialika vikubdi mbalimbali vya jogging vilivyopo ndani ya jiji ma kabla ya kuanza michezo ya mpira wa miguu na Pete, tutaanza kukimbia umbali mfupi wa km 4 au 5, ili tusiwachoshe wachezaji wetu" amebainisha.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments