CCM WILAYA YA IKUNGI YATAKA HOSPITALI YA MAKIUNGU IPANDISHWE HADHI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akiwasalimia wanachama wa chama hicho wa Kata ya Makiungu na Mungaa baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya sherehe za CCM kutimiza miaka 46 sherehe zilizo fanyika Kata ya Makiungu ambazo ziliambatana na shughuli za kutembelea Hospitali ya Makiungu inayomilikiwa na Kanisa Katoliki na , kutoa msaada wa sabuni, mafuta ya kupaka, pipi na maji kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo na kupanda piti viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mungaa na kufuatia mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wa kata hizo na Wana CCM.

Na Dotto Mwaibale, Singida

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kimeiomba Serikali kuipandisha hadhi Hospitali Teule ya Makiungu inayomilikiwa na Kanisa la Katoliki Jimbo la Singida ili iwe na uwezo wa kupokea wagonjwa wa Bima ya Afya.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi MikaLikapakapa baada ya kuzungumza na Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Padri Alessandro Nava wakati wa ziara ya viongozi wa chama hicho kutembea hospitali hiyo kwa ajili ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika za kutoa matibabu kwa wananchi ambapo walitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa  ikiwa ni moja ya kazi ya uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe ya  CCM kutimiza miaka 46 tangu kuanzishwa kwake ambapo kilele cha sherehe hiyo kimkoa zitafanyika Februari 5, 2023 Kata ya Minyughe wilayani humo.

"Hosptali hii inatoa matibabu kwa gharama ya chini lakini mkurugenzi wake Padri Nava ametuambia wanashindwa kutoa matibabu kupitia bima ya afya kwa sababu bado haijapandishwa hadhi na sisi kama chama tutaipeleka changamoto hiyo Serikalini ili ifanyiwe kazi" alisema Likapakapa.

Katika hatua nyingineLikapakapa aliitaka serikali kurejesha ruzuku ya Sh.milioni 180 zilizokuwa zinatolewa awali katika Hospitali hiyo Teule ya Makiungu kwa kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaozaliwa katika hospitali hiyo ambao ni zaidi 400 kwa mwezi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Ally Mwanga walitoa ushauri huo jana Januari 30, 2023  baada ya kutembelea hospitali hiyo inayoendeshwa kwa ubia na serikali inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Singida.

Likapakapa amesema Sh.milioni 60 za ruzuku zinazotolewa sasa na serikali ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya akina mama wanaojifungua katika hospitali hiyo. Aidha, amesema hospitali hiyo ipandishwe hadhi kuwa hospitali ya rufaa na pia madaktari bingwa wanaokuja kutoa huduma kwenye hospitali kutoka nje wasiwe wanapewa usumbufu.

Viongozi na wanachama hao walitembelea hospitali hiyo kuwafariji na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wazazi ambapo zawadi walitoa ni sabuni za kuogea na kufulia, mafuta kupaka,maji ya kunywa, biskuti na pipi.

Baada ya kutembelea hospitali hiyo Wana CCM hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao Likapakapa walikwenda Shule ya Sekondari ya Mungaa na kupanda miti na baadae  kufanya mkutano wahadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi pamoja na wanachama wa chama hicho.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mwenyekiti Likapakapa aliwaomba wanananchi na Wana CCM kuendelea kuwa na imani na CCM kwani ndio chama ambacho kimewaletea maendeleo makubwa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasije wakababaishwa na mtu yeyote.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akizungumza kwenye mkutano huo alisema chama hicho kimefanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi hivyo wasije wakatokea watu kutoka vyama vingine na kuanza kuwaongopea kuwa hakuna kilichofanyika.

"Wakitokea watu hao na kutaka kuwarubuni wapuuzeni kwani hawana jipya la kuwaambia kwani baadhi yao waliwahi kuwa viongozi wa wilaya hiyo lakini walishindwa'' alisema Mtaturu huku akishangiliwa na wananchi.  

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akitoa msaada wa maji, biskuti na sabuni kwa mgonjwa aliyelazwa kwenye Hospitali ya Makiungu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa (kushoto) akisalimiana na Mbungewa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ikungi, Nasoro Henku akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbola Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akihutubia katika mkutano wahadhara.

Msanii OmariIkimbia na MbungeMtaturuwakionesha umahiri wa kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wanyaturu. 

Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendego akizungumza kwenye mkutano huo.
Shamrashamra wakati wa kwenda kutembelea Hospitali ya Makiungu kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali.


Kada wa CCM, Daudi Kijangai akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendegoakisalimiana na Mkurugenzi wa Hospitali ya Makiungu Padri Alessandro Nava baada ya kuwasili katika hospitali hiyo kuwafariji wagonjwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya yaMkalama, Ally Mwangu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza na  Hospitali ya Makiungu Padri Alessandro Nava.
Mtunza stoo ya dawa wa hospitali hiyo Dk. Manuela Buzzi akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Wilayaya Ikungi Mika Likapakapa wakatiwalipotembelea hospitali hiyo kuona jinsi uhifadhi wa dawa unavyofanyika.
Ziarakatika hospitali hiyo ikiendelea.
Wagonjwa wakisubirikupata matibabu kwenye hospitali hiyo
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Maria Cornel akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa.
Mwenyekiti wa CCM Mika Likapakapa akiwafariji wagonjwa katika hospitali hiyo.
Vitu mbalimbali vikikabidhiwakwa wagonjwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri yaWilayaya Ikungi, Ally Mwanga akitoa msaada kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Msaada ukitolewa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa ChamaCha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Zilfat Muja akitoa msaada kwa mgonjwa.
Msaada kwa wagonjwa ukitolewa.
Kada wa CCM Rebeca Rahmajr akitoa msaada kwa mgonjwa.
Kada wa CCM Rebeca Rahmajr akiwa amembeba mtoto wakati wa ziara hiyo.
Misaada ikitolewa
Ziara ikiendelea.
Ni furahatupu wakati wa ziara hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mika Likapakapaakipeana mkono na Muuguzi wa zamu MariaCornel.
Zawadii zaidi zikitolewa.
Picha ya pamoja baada ya kutembelea hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akipanda mti katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mungaa.
Miti ikipandwa.
Miti ikipandwa.
Miti ikipandwa.
Wana CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Taswira ya mkutano huo.

Msanii Omari Ikimbia akionesha umahiri wa kucheza na kugani nyimbo za Kinyaturu.

Viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo wakiimbiwa wimbo maalumu wa kabila la Wanyaturu na wakina mama wa CCM wa wilaya hiyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments