Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana ameliagiza Baraza la Michezo nchini (BMT) kusimamia vyema Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya kutekeleza suala la michezo katika maeneo yao.
Mhe. Chana ametoa agizo hilo Februari 20, 2023 wakati alipofanya kikao cha kwanza na Baraza hilo tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo.
"Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya chini ya Makatibu Tawala lazima zihakikishe michezo inachezwa, miundombinu inaboreshwa na kusimamiwa vyema ili watoto wetu wacheze na hatimaye tupate vijana wazuri katika timu ya Taifa," amesisitiza Mhe. Waziri Chana.
Ameipongeza BMT kwa kutekeleza maagizo ya Rais wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha Tamasha la Michezo la Wanawake ambalo tayari limeshafanyika kwa miaka miwili mfululizo.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Neema Msitha ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha Bajeti ya Baraza hilo ambayo imesadia kuleta mageuzi katika kuendeleza michezo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri aliongozana na Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu, Bw. Saidi Yakubu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay na Katibu Mtendaji wa BMT.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumzana Watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, mara baada ya kufanya ziara katika ofisi zao zilizopo Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam Februari 20, 2023.
0 Comments