DIWANI KATA YA MIKOCHENI AKUTANA NA WANANCHI MTAA WA DARAJANI KUSIKILIZA KERO ZAO

Diwani wa Kata ya Mikocheni Eng Hussein Nzenzely amekutana na Wananchi wa Kata ya Mikocheni Mtaa wa Darajani kwaajili ya kusikiliza kero ambazo wanakabiliana nazo pamoja na kupokea ushauri.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Mratibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Kinondoni OCD Almachius Mchunguzi,Afisa mtendaji wa kata,Afisa maendeleo wa Kata , Mwenyekiti wa Mtaa,Mtendaji wa mtaa pamoja na wananchi wa kata ya Mikocheni.

Diwani wa Kata ya Mikocheni Eng Hussein Nzenzely akiongea wakati alipokutana na Wananchi wa Kata ya Mikocheni Mtaa wa Darajani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Sehemu ya wa ananchi wa Kata ya Mikocheni Mtaa wa Darajani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam katika m kutano huo.


Mratibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Kinondoni OCD Almachius Mchunguzi akiongea katika kikao hicho

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments