Gekul Awataka Wazalishaji Wa Maudhui Kuzingatia Utamaduni Wa Kitanzania

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amewataka waandaaji na wazalishaji na waandaaji wa maudhui kuzingatia mila na desturi za Tanzania.


 Mhe. Gekul ametoa Rai hiyo Februari 14, 2023 jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji  Tanzania.
 
Amesema kuwa ni jukumu la wadau hao wa utangazaji kuchuja maudhui kabla ya kuyafikisha kwa jamii ili yasilete athari za kudidimiza utamaduni wa Taifa.
 
"Vyombo vyenu visiiwe chanzo cha kubomoa utamaduni wetu, tuwe na mipaka nini tuipe jamii na nini tusiipe, tusikope mila za watu wengine ambazo hazina mwelekeo na utamaduni, na zaidi sana tuandae maudhui ambayo yatasaidia kulinda mila na desturi zetu," amesisitiza Mhe. Gekul.
 
Aidha, amewataka wadau hao kutumia nafasi zao katika kukuza maudhui ya ndani ikiwemo sanaa, filamu, muziki, sanaa za maonesho ambazo  zinazozalishwa ndani ya jamii husika.

 Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari  amesema mkutano huo  unalenga kubadlishana uzoefu miongoni mwa wazalishaji wa maudhui  katika kuzalisha maudhui bora ya ndani.

 Mkutano huo wa siku mbili umeshirikisha wadau mbalimbali wanaozalisha maudhui na umeongozwa na Kauli mbiu "Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza Uchumi wa Kidijitali"



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments