GGML KUWAPATIA MAFUNZO KAZI WAHITIMU 50 WA VYUO VIKUU NCHINI

JESHI la Polisi Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wameahiriki kufanya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wananchi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Akizungumza baada ya kushiriki kwenye usafi,Kamanda wa Polisi Wilaya ya Same SSP Phinias Majula asema wao kama jeshi la polisi wameona ni vyema kushirikiana na jamii kwenye kusafisha mazingira kuepuka milipuko ya magonjwa kama kipindupindu, lakini mazingira yanakuwa safi na salama.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi kuendelea  kutunza mazingira  ili yawe safi  huku akitumia nafasi hiyo kuomba jamii  kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taharifa za uhalifu katika wilaya hiyo, kwani ni jukumu lao kuwalinda wananchi na mali zao. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Mji Mdogo Wilaya ya Same akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Anastazia Tutuba ametoa shukrani za dhati kwa Jeshi hilo kwa  kushirikiana na wananchi kwenye shughuli za kijamii.

pia ameliomba kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na wananchi kwa  lengo ni kujenga usiano mzuri baina ya jeshi na wananchi.Chanzo Michuzi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments