Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata akizungumza kwenye kikao hicho alipongeza ushirikiano uliopo baina ya watendaji wa Serikali na chama hicho na kwamba hata miradi iliyotembelewa na kamati ya siasa ya mkoa inakwenda vizuri.
Aidha Bi Martha Mlata aliwataka wabunge kuacha kuwatishia wakuu wa wilaya na wakurugenzi na kwamba kunapokuwa na changamoto yoyote wafuate taratibu,
Wakati huo huo aliwaeleza wajumbe Wa Kikao hicho kuwa watendaji wanaletwa kwenye mkoa wetu ili watusaidie, kuleta maendeleo kwa faida yetu sasa na vizazi vijavyo tunatakiwa tuwape ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao vyema” alisema Mlata.
Kwa Upande Wa Mkuu Wa Mkoa Wa Singida Bw. Piter Serukamba amesema tunapaswa Kuache majungu na uongo ilikuendeleza umoja wetu kwakufanya kazi kwa bidii na kumuunga mkono kwa dhati Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassani Kwajili ya maeendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
0 Comments