Kamati za Bunge zapata viongozi, wengine watetea nafasi zao

Siku chache baada ya Spika wa Bunge kufanya mabadiliko katika kamati za kisekta na kuongeza idadi ya kamati kutoka tisa hadi 11, leo wamechagua huku wengine wakirejea katika nafasi zao.


Wajumbe wa Kamati za Bunge wamefanya uchaguzi wa kuwachagua wenyeviti na makamu wao ambapo wengi wamefanikiwa kutetea nafasi zao licha ya mabadiliko ya muundo wa kamati za kisekta.

Uchaguzi umefuatia muda wa uhai wa kikanuni wa kamati hizo wa mikutano 10 ya Bunge kumalizika.

Waliotetea nafasi zao katika kamati walizokuwa wakihudumu ni Naghenjwa Kaboyoka Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Halima Mdee katika Kamati ya Serikali za Mitaa (LAAC), Daniel Sillo wa Kamati ya Bajeti na Dastan Kitandula wa Kamati ya Nishati na Madini.


Wengine waliotetea uenyekiti ni kamati ya Miundombinu, Moshi Kakoso, Dastan Kitandula (Nishati na Madini), Jasson Rweikiza (Sheria Ndogo), Jerry Silaa (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) na Vita Kawawa (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama).

Wenyeviti waliosalia katika nafasi ya uenyekiti licha ya kamati zao kufanyiwa mabadiliko ni Fatma Tofiq (Ustawi na Maendeleo ya Jamii), Dk Joseph Mhagama (Utawala, Katiba na Sheria), David Kihenzile (Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo), Stanslaus Nyongo (Afya na masuala ya ukimwi) ambayo awali ilikuwa katika Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imegawanya katika kamati mbili ambazo ni Afya na Masuala ya Ukimwi pamoja na Elimu, Utamaduni na Michezo.

Wenyeviti wapya na kamati zao katika mabano ni Profesa Kitila Mkumbo (Elimu, Utamaduni na Michezo), Denis Londo (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Jackson Kiswaga (Maji na Mazingira). Timotheo Mzava (Ardhi, Maliasili na Utalii).

Kamati ya Bunge ya Haki, Madaraka ya Bunge itaongozwa na Ali Juma Makoa ambaye awali alikuwa ni mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


Kwa upande wa makamu wenyeviti wanaorejea na kamati zao katika mabano ni Mariam Ditopile (Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo), Vicent Mbogo (Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama), Omary Kigua (Bajeti), Japhet Hasunga (PAC), Stanslaus Mabula.

Wapya ni Florent Kyombo (Utawala, Katiba na Sheria), Lazaro Nyamoga (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Riziki Lulida (Ustawi na Maendeleo ya Jamii), Anna Lupembe (Maji na Mazingira) pamoja na Husna Saiboko (Elimu, Utamaduni na Michezo).

Wengine ni Ally Makoa (Ardhi, Maliasili na Utalii), Dk Faustine Ndugulile (Afya na masuala ya Ukimwi), Anne Malecela (Miundombinu), Judith Kapinga (Nishati na Madini), Ramadhan Ramadhan (Sheria Ndogo) na Dk Thea Ntara (Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments